Makala hii inatumwa kwa watu 51,522 walijisajili
Barua pepe yako kama haionekani vizuri, fungua hapa kwenye browser
Tamasha la tisa la Sauti za Busara litafanyika mji mkongwe Zanzibar kuanzia tarehe 8 jumatano– 12 jumapili ya mwezi wa pili 2012. 100% LIVE African music under African skies.
Sauti za busara huwaleta watu pamoja kusheherekea, muziki tofauti na ladha za muziki kutoka afrika mashariki na kwingineko.
Tamasha litazinduliwa rasmi na Maandamo makubwa yatakayozunguka mitaa ya Zanzibar yatakayo shirikisha vikundi tofauti kama beni brass bendi,wapiga ngoma, mwanandege, wacheza sarakasi nk ndani ya Ngome kongwe vikundi vya muziki kutoka shemu zote za afrika vitafanya maonyesho kila siku kuanzia saa 11 jioni mpaka saa 7 usiku. Baada ya jua kuzama program ya filamu za muziki wa kiafrika itaanza rasmi na video za muziki, makala na Tamasha likiendelea. Vyakula vya kizanzibar, vinywaji, muziki, vito, nguo na vinyago vipo karibu na tamasha. Wakati huo huo kutakuwa na matukio tofauti yakiendelea nje ya tamasha kama ngoma, maonyesho ya mavazi, mashindano ya ngalawa na matukio mbalimbali.
Baadhi ya wasanii waliothibitisha kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2012 ni:
Ally Kiba (Tanzania) Super Mazembe (DRC / Kenya) Nneka (Nigeria) Tumi & The Volume (South Africa) Seven Survivor (Tanzania) Ary Morais (Cape Verde) Chébli Msaïdie (Comoros) EJ von Lyrik(South Africa) Companhia Nacional de Canto e Danca (Mozambique) Ndere Troupe (Uganda) Teba Shumba (South Africa) Ogoya Nengo (Kenya) Kidumbaki JKU (Zanzibar) Skuli ya Kiongoni (Zanzibar) Lumumba Theatre Group (Tanzania) Tausi Women's Taarab (Zanzibar) Kozman Ti Dalon (Reunion) Qwela (Uganda) Shirikisho Sanaa (Zanzibar) Swahili Vibes Band (Zanzibar) Tunaweza Band (Tanzania) Jembe Culture Group (Tanzania) Hanitra (Madagascar) Leo Mkanyia (Tanzania) Tandaa Traditional Group(Zanzibar) Utamaduni JKU (Zanzibar) Wanafunzi wa SOS (Zanzibar) na wengineo wengi kuthibitishwa
![]() |
![]() |
![]() |
EJ von Lyrik (South Africa) |
Ally Kiba (Tanzania) |
Nneka (Nigeria) |
Ratiba inaweza kubadilika kutokana na uthibitisho kutoka kwa wasanii. Tembelea www.busaramusic.org/festivals/2012 kwa maelezo zaidi.
Tembelea makala mpya kwenye tovuti yetu kama ifuatavyo chati ya muziki ,matamasha ya muziki yanayofanya vizuri , Kalenda ya matukio ya sanaa Afrika mashariki, picha na video
Ngome kongwe kuna kiwango maalum. Ili uwe huru na uhakika wa kuwepo katika tamasha unashauriwa kununua pasi ya tamasha zima mapema kabla ya mwisho wa mwezi wa kwanza. Ukiwa na pasi ya tamasha zima utazawadiwa kitabu cha maelezo kuhusu Tamasha.Wekesha tiketi yako kupitia hapa:ZANZIBAR-ISLANDS.COM
Tunatafuta wataalam wa muziki wa kiafrika wenye hadithi za mafanikio ili kubadilishana mawazo katika semina yetu ijayo ndani ya mji mkongwe Zanzibar mwezi wa pili 2012.
Semina ni changamoto, ni mkutano rasmi kwa wataalam wa muziki wa ndani na wa nje kukutana na kujadiliana katika kipindi cha Tamasha. Vikao vitaanza kila siku kuanzia saa 9 mpaka saa 11 jioni kwa majadiliano kwa washiriki, kubadilishana taarifa na kutoa mawazo ya kuendeleza sanaa ndani ya afrika mashariki na kwingineko.
Semeina hii ni bure na mlango upo wazi kwa wasanii, mameneja, mapromota, waandishi wa habari, wachangiaji, wadhamini na wataalam wa sanaa.
Kama una hadithi ya kusisimua na unataka kushiriki wasiliana nasi kwa barua pepe busara@busara.or.tz
Tunatafuta aina mbalimbali ya filamu zenye kusisimua na kuburudisha ili ziweze kuonyeshwa, kutoka bara la afrika na nje. Inaweza ikawa makala ndefu, matamasha yaliyorekodiwa. Filamu tunazotafuta lazima ziwe na sifa zifuatazo:
> Filamu zenye muonekano mzuri, ubora wa sauti na muziki wenye asili ya Kiafrika
> Filamu zinazoelezea ujio mpya na sauti zisizosikika na wasanii chipukizi
> Filamu za muziki ambazo zinaelezea ubora na utofauti ndani ya afrika mashariki na kwingineko.
Filamu za kutoka nje ziwe zenye tafsiri ya Kiswahili au kingereza
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 18 Novemba 2011.
Kwa maelezo zaidi na fomu za maombi tembelea www.busaramusic.org/callforfilm
Kama una maoni, tovuti, au filamu ya muziki wa kiafrika tujulishe kwa kupitia barua pepe ifuatayo busara@busara.or.tz
Je unatafuta kampuni ya kuaminika ili kuandaa safari yako kuja kwenye tamasha? Jaribu Songlines Festival Tours (Ulaya)au Zanzibar Festival Tours ( America ya kusini)
Kwa taarifa zaidi kuhusu kuja Zanzibar tafadhali wasiliana na Tabasam Tours
Maelezo zaidi kuhusu utalii wa Zanzibar na punguzo kwa ajili ya tamasha tambelea Taarifa kwa wageni
Angalia kipindi live katika televisheni katika miaka ya themanini ambayo imebadilisha maisha ya mwingereza, Yusuph Mahmoud. Miaka hiyo Bw yusuf alikuwa anafanya kazi ya kuuza maziwa ndani ya Cheltenham na kujishughulisha kidogo na kazi ya Udj, lakini baada kugundua kuwa muziki unaweza kuwa chombo cha mabadiliko alijihusisha na shughuli za uendelezaji wa muziki katika kupambana na ubaguzi wa rangi na shughuli zingine.
Baada ya miaka kadhaa, alifanikiwa kupata nafasi ya kufanya kazi katika tamasha la kwanza la filamu la kimataifa (Zanzibar international film festival). Kutokana na mapenzi yake kwa muziki wa kiafrika, alikusudia kukaa zanzibar kwa miezi sita. Miaka kumi na tatu sasa, yupo zanzibar na ameanzisha tamasha la sauti za busara- kustawisha tamasha ambalo linasaidia muziki wa afrika mashariki...soma zaidi / sikiliza hapa
Yusuf na Rosie kutoka Busara Promotions watakuwa WOMEX katika mji wa Copenhagen kuanzia tarehe 26 -30 Oktoba.
Tutembelee WOMEX Stand M.07
Sauti za Busara itafanya mkutano na wadau. Mkutano utawaleta pamoja wawakilishi wote kutoka katika sekta za Umma , binafsi na serikali kwa ujumla, sekta ya utalii, wafanyabiashara, wasimazi wa sanaa ili kuchunguza athari za matamasha zanzibar, kuimarisha ushirikiano na kujenga urafiki.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia busara@busara.or.tz
Waandaaji wa tamasha wanayofuraha kukiri imani yao, maono yao na misaada madhubuti kutoka kwa wafadhili na wadhamini, bila ya wao tamasha la sauti za busara lisingeweza kufanyika. Katika kipindi hiki cha matayarisho, bajeti na mipango inatupa wakati mgumu wa kutokulala usiku. Tumepokea ahadi chache na bado tunahitaji zaidi kabla ya kila kitu kuthibitishwa kwa 100%.
Mpaka sasa sauti za busara 2012 imewezeshwa na :
Principal Donors
|
||||
![]() |
||||
Main Donors |
||||
|
||||
Sponsors |
||||
|
||||
Donors |
||||
![]() |
||||
Media Partners
|
||||
|
||||
Zanlink, Multi-Color Printers, Tabasam Tours, Emerson Spice, Monsoon Restaurant, Mercury's, Archipelago Restaurant, Stone Town Café, www.zanzibar.net
Kama unataka nembo yako kuingizwa kwenye habari zetu zitakazofuata bofya hapa
![]()
|
Busara Promotions
Tunapatikana barabara iendayo Uwanja wa ndege, mkabala Golf Club Tel: +255 24 223
2423 |
Please forward this mail to friends who may be interested. To subscribe or unsubscribe to our newsletter – just type your email address in the box at |