|
Jarida hili linatumwa kwa watu 57,789
|
|
|
|
|
Usijibu kutumia barua pepe hii. Kama utapenda kuwasiliana nasi tafadhali tumia busara@busara.or.tz |
|
|
|
|
Mwisho wa wito wa wasanii: Sauti za Busara 2013 |
Top |
|
Sauti za Busara ni tamasha la muziki namba 1 Afrika Mashariki. Tamasha la 10 litafanyika Zanzibar ndani ya mji mkongwe katika ukumbi wa Ngome Kongwe kuanzia tarehe 14 - 17 februari 2013.
Sheherekea hazina ya muziki wa kiafrika, tamasha litaonyesha wasanii bora, wanaofanya maonyesho yao moja kwa moja kwa asilimia 100 (live), kutoka ijumaa mpaka jumapili, saa 11 mpaka saa 7 usiku. Na mengineyo zaidi ikiwemo filamu za muziki wa afrika, vyakula kutoka kwa wenyeji na maduka ya sanaa, warsha kwa ajili ya kuongeza ujuzi, mikutano ya wataalam wa sanaa, na vilevile Matukio ya ziada ya busara yahusuyo muziki na mambo ya utamaduni yatakayoandaliwa na wenyeji na kufanywa katika sehemu mbalimbali za mji wa Zanzibar.
Wanamuziki wa kiafrika kutoka sehemu yoyote duniani wanakaribishwa kufanya maombi ya ushiriki kwa ajili ya kufanya maonyesho yao katika jukwaa la sauti za busara, kwa kukamilisha maombi kwenye mtandao na kutuma nakala za kazi ambazo zitufikie kabla ya tarehe 31/7/2012. Kamati ya uchaguzi itafanya uteuzi mwezi wa nane na mwezi wa tisa wasanii wote waliochaguliwa watajulishwa.
 |
Sauti za Busara 2013 postcard |
|
|
| |
|
Pati ya shukran kwa Marafiki wa Busara |
Top |
|
Kwa kuwashukuru marafiki wa busara na wale wote waliosaidia tamasha la busara 2012, tunaandaa pati katika ofisi za busara siku ya ijumaa ya tarehe 22 ya mwezi wa sita. Kutakuwa na nakala ya filamu “More than a festival” bila shaka tamasha linaleta mapinduzi ya kimuziki, shamrashamra na mkusanyiko wa watu.
Kwa mualiko tu! Barua pepe busara@busara.or.tz kama unahitaji mualiko. |
 |
Nighttime Audience (photo: Robin Batista) |
|
|
|
| |
|
Wito kwa wahisani & wadhamini wa tamasha |
Top |
|
-(6).gif) |
Busara on stage (photo: Stephanie-Tinga-Baron-Wilson) |
|
Tiketi za tamasha kwa kila siku ni shilingi 3000 kwa mtanzania. Katika kusaidia uwepo wa tamasha tunategemea michango kutoka kwa wahisani na wadhamini.
Tamasha linathamini wahisani na wadhamini wote waliopo katika tovuti ya sauti za busara (mwezi wa januari tu tovuti ya www.busaramusic.org ilitembelewa mara milioni 3.4) vilevile na jarida (kutumwa kwa watu 57,000 dunia nzima) na kitabu cha tamasha, mabango ya matangazo, matangazo ya jukwaani, taarifa kwa vyombo vya habari na mengineyo…
Kama unapendelea kuwa rafiki na tamasha, barua pepe marketing@busara.or.tz kwa taarifa zaidi |
|
|
| |
|
|
Mkurugenzi mtendaji, Busara Promotions
Muda wote, mkataba wa miaka miwili, kuanza tarehe 6/8/2012. Kutoka taifa lolote (mwenye uzoefu angalau wa miaka 3 kwenye NGO / uongozi wa sanaa). Mwenye kuwajibika katika shughuli za utawala na fedha wa NGO. Tuma barua na CV yako kwa director@busara.or.tz kabla ya tarehe 30/06/2012.
Kwa taarifa zadi bonyeza hapa |
Meneja wa ufundi, Busara Promotions
Muda wote, mkataba wa miezi sita, kuanza tarehe 1/10/2012. Kutoka taifa lolote (mwenye uzoefu angalau wa miaka 5). Kuwa mwenye dhamana ya kutoa msaada wa kiufundi kwa Sauti za busara na miradi mingine. Tuma barua na CV yako kwa director@busara.or.tz kabla ya tarehe 31/07/2012.
Kwa taarifa zadi bonyeza hapa |
Ofisa habari,Busara Promotions
Muda wote, mkataba wa miezi sita, kuanzia tarehe 1/10/2012. Kutoka Tanzania na Afrika Mashariki. Tuma CV yako na barua kwa busara@busara.or.tz kabla ya tarehe 31/07/2012.
Kwa taarifa zadi bonyeza hapa |
|
 |
Lighting work (photo: Masoud Khamis) |
 |
Backstage soundbooth (photo: Masoud Khamis) |
|
Busara Promotions inazingatia usawa wa kijinsia katika nafasi za kazi kwa wenyeji vyovyote iwezekanavyo.
Tafadhali zingatia muombaji atakayekuwa makini pekee ndiyo. |
|
|
| |
|
Uzinduzi wa CD: Bongo Hotheads |
Top |
|
 |
Jagwa Music Bongo Hotheads CD cover |
|
Kutoka katika kitongoji cha Mwananyamala ndani ya jiji la Dar es salaam, wanafahamika kwa jina Jagwa Music hufanya maonyesho yao ya kuvutia, mpiga kinanda huwapagawisha watu zaidi na kinanda chake aina ya Casio na watu watatu wakiwa mbele, wachezaji wawili na muimbaji, akishusha nyimbo zinazoelezea maisha ya mjini, usaliti katika mapenzi na ushirikina. Tazama filamu kutoka YouTube hapa
Jagwa Music si tu wana umaarufu katika viunga vya Dar es Salaam lakini wameweza kuvuta hisia za watu katika tamasha kubwa la kimataifa barani ulaya Roskilde Festival. Kwa mara ya kwanza Cd yao inapatikana kimataifa, "Bongo Hotheads" wametoa utajiri wao wa mashairi. Pata nakala yako maridhawa sasa.
"A spirited, exuberant debut like nothing you’re likely to have heard before" (The Arts Desk) |
|
|
| |
|
Kalenda ya matamasha Zanzibar |
Top |
|
Tamasha letu si pekee ndani ya mji mkongwe:
15th ZIFF Festival of the Dhow Countries:
7 - 15 July, 2012
Tamasha kubwa la filamu na sanaa Afrika Mashariki, wanatoa wigo mpana wa ubunifu ndani ya Afrika na nje ya Afrika. Soma hapa
|
2nd Jahazi Literary and Jazz Festival:
31 Aug – 2 Sept, 2012
Mwisho wa wiki maridhawa wa ufunguzi wa tamasha la Jahazi, simulizi za hadithi, usomaji wa mashairi, semina za muziki na chakula cha join kwa VIP... Soma zaid
|
|
 |
Daytime Audience (photo: Pernille Barendtsen) |
|
Angalia kalenda kwa Matukio ya sanaa Afrika Mashariki
Angalia kalenda kwa Matamasha ya Muziki Afrika |
|
|
| |
|
|
|
www.busaramusic.org |
Busara Promotions
PO Box 3635
Stone Town
Zanzibar,
Tanzania
Tunapatikana barabara iendayo uwanja wa ndege, mkabala na Golf Clubb
busara@busara.or.tz
Tel: +255 24 223
2423
or +255 773 822 294 |
|
Tafadhali itume barua pepe hii kwa marafiki ambao wangependelea kuipata. Kujiunga au kujitoa andika barua pepe yako katika chumba katika
www.busaramusic.org |
|
|
| |
|
|