Sauti za Busara 2017

inaandaliwa na Busara Promotions, NGO iliyosajiliwa Zanzibar. Tamasha la Sauti za Busara ni miongoni mwa matamasha yanayoheshimika Afrika ‘Africa’s best and most respected music events’(BBC World). Baada ya kutokuwepo kwake kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, Sauti za Busara inarudi tena ndani ya viunga vya Mji Mkongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 9– 12 Februari 2017. Orodha kamili ya wasanii na matukio mengine yatatangazwa rasmi mwezi wa Oktoba. Siku nne za tamasha matukio mbalimbali yatachukua nafasi:

  • Muziki wa Moja kwa Moja: Music bora kutoka kwa wasanii 400, Vikundi 40 jukwaani vikipiga laivu!
  • Maonyesho ya Barabarani & Matembezi: Vionjo mbalimbali katika maeneo ya mjini na viunga vyake!
  • Swahili Encounters: Ushirikiano kati ya wasanii wageni na wenyeji
  • Movers & Shakers: Mkutano wa wataalamu wa ndani na nje katika tasnia ya sanaa ya muziki
  • Busara Xtra: Matukio mbalimbali yanayoandaliwa na wenyeji

Sauti za Busara inaonyesha muziki bora na wenye utambulisho wa Afrika, na wakati huohuo:

  • Inahamasisha amani na kuheshimiana
  • Huongeza ajira na kuboresha maisha
  • Hutoa ujuzi na fursa za kujifunza
  • Husaidia kukuza uchumi kwa jamii
  • Kulinda uhuru wa kujieleza


Tiketi & Pasi

AFRICA UNITED Punguzo Maalum kwa waafrika. Raia wa Nchi za Afrika ni nusu bei,Punguzo la nguvu kwa Watanzania