Usijibu kwa barua pepe hii. Kwa mawasiliano nasi [email protected]. Tafadhali watumie marafiki watakaopendezwa na jarida hili.
|
|
|
Paza sauti za wanawake: Sauti za Busara 2022
|
|
|
Salam nyingi kutoka Mji Mkongwe, Zanzibar! Tamasha la Sauti za Busara 2022 lilifanyika kwenye viunga vya Mji Mkongwe aka Old Fort kuanzia Ijumaa, tarehe 11 mpaka Jumapili, tarehe 13 Februari. Tamasha lilionyesha dunia sura ya Tanzania na Afrika ambayo mara nyingi haionekanihuku takribani watu 4,000 wakihudhuria kila siku kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika, na mabara mengine na kuungana kwa lengo moja tu la kusheherekea muziki mubashara kutoka Tanzania, Uganda, Zimbabwe, Zambia, Congo, Reunion na Afrika ya Kusini.
Janga la UKIVO-19 limeathiri safari za kimataifa kwani nchi nyingi bado zinaweka masharti magumu dhidi UVIKO. Hata hivyo, licha ya changamoto hizi na nyinginezo za kifedha, tulifanikiwa kufanya tamasha ambalo watu wengi wanasema ni tamasha letu bora zaidi hadi sasa!
Kwa mara nyingine tena, tulithibitisha kuwa watazamaji wanatamani maonyesho mbalimbali ya muziki kutoka barani Afrika. Tulionyesha kuwa inawezekana kuandaa tamasha la kipekee la muziki wa Kiafrika ambalo huleta manufaa na mafanikio ya kijamii na kiuchumi kwa kisiwa hiki, lakini bila kuathiri urithi wetu wa kitamaduni.
Macho yetu mwaka huu yaliangazia wasanii wa kike kutoka Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika, chini ya kauli mbiu ‘Paza Sauti; Amplifying Women’s Voices’. Pia katika idara nyingine, wafanyakazi wa kike waliajiriwa kama waratibu, mafundi, wasimamizi wa jukwaa na wafanyakazi wa usalama, kwa kutambua kwamba fursa kwa wanawake zinahitaji kuongezwa katika sekta zote za tasnia ya muziki.
|
|
|
Sauti za Busara 2022 Wamwiduka Band (Tanzania) audience (photo Massoud Khamis)
|
|
Sauti za Busara 2022 Nomfusi (South Africa) audience (photo Markus Meissl)
|
|
|
Sauti za Busara 2022 Msaki (South Africa) audience (photo Rashid Nadhir)
|
|
Sauti za Busara 2022 Zan Ubuntu Band (Zanzibar) (photo Rashde Fidigo)
|
|
|
Sauti za Busara lamalizika kwa mafaniko mjini
|
by DW Kiswahili, 14 Feb 2022
|
|
|
|
|
Mwisho kabisa, shukrani nyingi ziwaendee wafadhili wote, wahisani, washirika, marafiki na wanafamilia wote kwa msaada yao ya hali na mali.
|
|
|
|
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
|
|
|
|
RVS TV, Emerson Zanzibar, Zanlink, Zanzibar Cable TV, Plus Radio, 2Tech Security, Zanzibar International Film Festival, DCMA Zanzibar, Kumi Gifts & Treats, Archipelago Waterfront, Café Foro, Stone Town Café, Hotel Maru Maru, La Taverna, Mercury’s Restaurant, Swahili Soft Technologies, Six Degrees South, ZMMI, Mozeti Tours, Azam Marine, Alliance Française Dar, Music In Africa, United Petroleum, Dar Life, ZANREC
|
|
|
|
Busara Promotions P O Box 3635 Stone Town Zanzibar, Tanzania
Find us off the airport road, Maisara
Tel: +255 24 223 2423 or +255 773 822 294
|
|
|
Like and follow Sauti za Busara
|
Tafadhali sambaza kwa marafiki watakaopendezewa. Kujiunga au kujitoa kwenye jarida letu, andika barua pepe kwenda www.busaramusic.org
|
|
|
|