Soma kwa English | Kiswahili / français
Usijibu kupitia barua pepe hii. Kwa kuwasiliana nasi tafadhali tuma kwa [email protected] Unaweza kuwatumia ndugu na marafiki ikiwa wanapenda.
Barnaba Classic Tanzania Audiences at Sauti za Busara 2021 photo by Lorenzo Maccotta
Sauti za Busara ni tamasha bora la muziki wa Afrika linalofanyika Mji Mkongwe, Zanzibar kila mwezi Februari, tamasha hili limefanikiwa kuvutia maelfu ya wadau wa muziki kutoka kila pembe ya dunia. Waanndaaji kwa sasa wapo katka harakati za maandalizi ya Tamasha la 19 litakaloanza tarehe 11th – 13th February 2022..
Tunawahamasisha wasanii wote wanaopiga muziki wa kipekee, wa kuvutia na wenye muunganiko na bara la Afrika, Nchi za kiarabu na ukanda wa Bahari ya Hindi nao wanakaribishwa kufanya maombi.
Orodha ya wasanii itatolewa mwezi wa Oktoba. Tamasha litaonyeshwa mubashara katika vituo vya luninga na kwenye mitandao mbalimbali.
Hata hivyo, kwasasa tunaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya Janga la Korona ndani na nje ya nchi. Kipaumbele chetu cha mwanzo ni Afya ya wenyeji na wageni. Vitali Maembe Tanzania Audiences at SzB 2021 (by Link Reuben) Sauti za Busara 2021 audience (photo Lorenzo Maccotta) Dulla Makabila Tanzania Audiences at SzB 2021 photo (by Link Reuben)
Sauti za Busara huonyesha muziki bora kutoka Bara la Afrika, vilevile wasanii kutoka nchi ya kiarabu na ukanda wa bara la Hiindi nao wanakaribishwa kufanya maombi.
Vipaumbele vitatolewa kwa :
Muziki wenye muunganiko na Afrika, Nchi za kiarabu na Bahari ya Hindi Wasanii wanawake, au vikundi vinavyoongozwa na wanawake Wasanii vijana, wapya na wanaochipukia Muziki wenye ujumbe chanya na wenye faida kwa jamii Muziki wenye kufanywa mubashara!
Mwisho wa kupokea maombi yaliyokamilika ni tarehe 31 July 2021 (usiku). Kwa taarifa zaidi na linki ya fomu ya maombi, tembelea https://www.busaramusic.org/call-for-artists-2022.
Tafadhali hakikisha maombi yako yameambatanishwa wasifu wa msanii, nakala za kusikiliza (MP3) na video (MP4) ya onyesho lililofanywa mubashara, pichazenye ubora na au link ya kurasa yako ya Music in Africa. Jopo la uteuzi litapitia maombi yote yaliyokamilika na yaliyotumwa mpaka tarehe 31 July 2021.
Punguzo kubwa la tiketi litapatikana hivi karibuni mtandaoni, likijumuisha bei maalum kwa watanzania, wenyeji wa Afrika Mashariki na wenye hati za kusafiria za Afrika.
Kaa tayari kwa filamu nzuri na bora, maonyesho, semina na mengineyo. Itafanyika ndani ya Mjji Mkongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 21 – 25 July 2021, kauli mbiu ya tamasha la 24 ni ‘Sharing Our Heritage’. Urithi Huu Ni Wetu Sote! Kwa taarifa zaidi tembelea: www.ziff.or.tz
The Music In Africa Conference for Collaborations, Exchange and Showcases (ACCES) inawaalika wanamuziki wa Afrika waliopo katika bara la Afrika kufanya maombi ya ushiriki katika ACCES 2021 jijini Johannesburg, Afrika Kusini, kutoka 25 mpaka 27 Novemba. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25 July 2021 (usiku CAT). Kwa taarifa zaidi na linki ya maombi, tembelea https://www.musicinafrica.net/acces
Tamasha la Sauti za Busara limeweza kufanyika kwa msaada mkubwa kutoka kwa ubalozi wa Norway Dar es Salaam ambaye anadhamini Busara Promotions kwa mwaka mzima Fursa za matangazo ya kiudhamini yatatolewa kwa kila muhisani na mdhamini. Tafadhali unaweza kuwasiliana nasi kama unapendelea kuwa mdhamini wa Sauti za Busara 2022.
Busara Promotions Find us off the airport road, Maisara Tel: +255 242 232 423 Follow us @sautizabusara Sauti za Busara official YouTube playlist Tafadhali shea jarida hili kwa yeyote anayependelea. Kujisajili ai kujitoa kwenye jarida letu, unaweza kuandika barua pepe yako kwenye kiboksi kilichomo ndani ya tovuti yetu www.busaramusic.org |