Usijibu kwa barua pepe hii. Ili kuwasiliana nasi, tafadhali tumia [email protected]
Tafadhali watumie jamaa na marafiki watakaopendezwa na jarida hili. |
Wito kwa Wasanii: Sauti za Busara 2023 |
|
|
Sauti za Busara 2023: Wito kwa Wasanii |
Fomu ya maombi kwa wasanii: Sauti za Busara 2023
Maombi ya wasanii yamefunguliwa rasmi kwa ajili ya tamasha la 20 la Sauti za Busara ambalo litarindima katika kuta za Mji Mkongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 9 – 12 Februari 2023.
Sauti za Busara huonyesha muziki wa kipekee na anuai, kutoka bara la Afrika na kwingineko. Wanamuziki wanaowakilisha Nchi za Kiarabu na ukanda wa Bahari ya Hindi, nao wanakaribishwa kuomba.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31 July 2022. |
Vipaumbele vitatolewa kwa: |
- Muziki wenye vionjo vya Kiafria, Nchi za Kiarabu na Ukanda wa Bahari ya Hindi
- Wasanii wanawake, au vikundi vinavyoongozwa na wanawake
- Vijana wenye vipaji na wanaochipukia
- Muziki wenye ujumbe unaofaa kwa jamii
- Muziki unaopigwa mubashara kwa asilimia mia!
|
|
|
Sauti za Busara 2022: Tunakomaa! |
|
|
Audience at Sauti za Busara 2022 by Rashid Nadhir |
| Audience at Sauti za Busara 2022 by Markus Meissl |
| Audience at Sauti za Busara 2022 by Rashde Fidigo |
|
|
Tamasha la Sauti za Busara 2022 ilifanyika katika Mji wa Kihistoria wa Mji Mkongwe, Zanzibar kuanzia 11- 13 Februari, kwa kila siku ya tamasha mashabiki na watazamaji 4,000 kutoka sehemu mbalimbali Afrika, Ulaya na mabara mengine kwa pamoja walijumuika katika kusheherekea muziki wa Afrika kutoka kwa wasanii wa Tanzania, Uganda, Zimbabwe, Zambia, Kongo, Visiwa vya Reunion na Afrika ya Kusini.
Athari za Uviko-19 zilipelekea changamoto za safari za kimataifa kwa nchi nyingi kuendeleza sheria kali na miongozo ya Uviko kwa wasafiri. Hata hivyo, licha ya changamoto zote hizo, tumeweza kufanya Tamasha ambalo mpaka sasa watu wengi wanasema lilikuwa bora!
Kwa mara nyingine, tumeshuhudia watazamaji wanahitaji muziki wa kipekee kutoka bara zima la Afrika. Tumeonyesha kwamba inawezekana kuandaa tamasha ambalo linaleta faida za kijamii na kiuchumi kwa Zanzibar, bila ya kutishia kuharibu utamaduni wetu.
Mwaka huu Tamasha liliangazia zaidi wanamuziki wa kike kutoka Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika huku kauli ikiwa ‘Paza Sauti; Amplifying Women’s Voices’. Nyuma ya pazia, wanawake waliajiriwa kama waratibu, mafundi, mameneja wa jukwaa na walinzi, kwa kutambua kuwa fursa kwa wanawake zinahitaji kuongezwa katika sekta zote za tasnia ya muziki.
Chaguo la wengi kwa Sauti za Busara 2022 liliwajumuisha Sampa The Great (Zambia), Siti & The Band (Zanzibar), Msaki (Afrika Kusini), Sholo Mwamba (Tanzania), Vitali Maembe (Tanzania), Sjava (Afrika Kusini), Fanie Fayar (Congo), Nomfusi (Afrika Kusini), Wamwiduka Band (Tanzania) na wengineo. |
Watch video highlights: Sauti za Busara 2022: Amplifying Women’s Voices |
© Busara Promotions, CL Films |
|
|
Shukran maalum kwa Blue Amber Zanzibar |
|
|
Kila mwaka mwezi Februari tangu 2004, Sauti za Busara imevutia maelfu ya watu kutoka ndani na ulimwenguni kote kusheherekea utajiri na utofauti wa muziki wetu na urithi wetu. Tamasha lisingewezekana bila ya wahisani na wadhamini kama Ubalozi wa Norway ambao walisaidia gharama zote za kuendesha ofisi tangu mwaka 2009. Kwa kuwa udhamini wao unaisha mwezi Machi 2022, tumeshatumia muda mwingi kutafuta mdhamini mwingine bila ya mafanikio. Hatukukata tamaa ila muda ulikuwa unakwenda na ikafika muda tukaanza kupoteza matumaini ya uwezo wa kuendelea.
Hatimaye kama miujiza wakajitokeza Blue Amber Zanzibar wamekubali kuisaidia taasisi yetu ya Busara Promotions kwa kugharamia uendeshaji wa ofisi kwa miaka mitatu ijayo. Maneno hayawezi kuelezea furaha ya wafanyakazi wa taasisi wanayo kwa wakati huu, kwa kutambua kwamba tamasha sasa linaweza kuendelea. Furaha hii ipo kwa maelfu ya watanzania, wasanii na wapenzi wa muziki duniani kote.
Blue Amber ni moja ya miradi ya kimkakati kwa Tanzania uliopo, Matemwe, pwani ya Kaskazini-Mashariki mwa, Zanzibar. Mradi huu mkubwa unaotarajiwa kuwa kivutio kikubwa cha mapumziko na burudani Afrika na kujulikana kama uwekezaji mkubwa wa kimkakati Tanzania. “Sauti za Busara imetengeneza thamani ya uwekezaji katika utalii na kipato kwa wananchi, kupitia Sanaa ya muziki, wanafanyakazi wa tamasha na vyombo vya habari vinavyoitangaza Zanzibar”. Alisema, Mkurugenzi Mtendaji wa Blue Amber, Grant Anderson. “Tamasha sasa limekuwa moja kati ya nguzo muhimu za jukumu letu kijamii na ningependa kuwahakikishia Wazanzibari na dunia kwa ujumla kwamba Sauti za Busara itakuwa zaidi katika hadhi na sifa.”
Mwanzilishi wa Blue Amber Zanzibar, Saleh Said aliongeza kwamba “kama Mzanzibari nilisikitika kusikia Tamasha la Sauti za Busara halitoweza kuendelea tena kutokana na uhaba wa pesa. Itakua ni uzembe kuacha tamasha life ikiwa limeweza kubadili maisha ya watu mbalimbali na Zanzibar kwa ujumla. Tuna furaha kwamba udhamini wetu utawezesha tamasha kuendelea na mipango yake.”
“Tamasha la Sauti za Busara kwa miaka mingi limeweza kuwavutia maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja kisiwani kwetu. Tumeona ukuwaji wa uchumi wa Zanzibar kwa miaka kadhaa na moja ya kichocheo ni Tamasha hili. Ni jukwaa ambalo wasanii na wanamuziki wetu waliweza kuuonyesha ulimwengu utamaduni na urithi wa Zanzibar. Vilevile ni jukwaa la kujifunza kutoka kwa washiriki wa Nchi nyingine yale mazuri yanayosaidia jamii zetu kuwa na ubunifu na kuwa na Uhuru wa kujieleza,” alisema Naibu Katibu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zanzibar, Mheshimiwa Khamisi Abdallah Said. “Taarifa ya Blue Amber kusaidia kuendelea kwa Tamasha la Sauti za Busara imepokelewa kwa furaha na Wazanzibari wote,” aliongeza.
Team Busara inawashukuru sana Blue Amber kwa moyo waliounyesha wa kusaidia tamasha. Vilevile tunawataka viongozi mbaliambali wa Serikali, Wahisani wa Kimataifa, Wakurugenzi wa mabenki, makampuni ya simu, sekta ya hoteli na usafirishaji kuiga mfano wa Blue Amber. Kuwekeza kwenye sanaa na utamaduni, saidia matamasha kuwa endelevu, ungana mkono na wale wote wanaotunza urithi wetu na kutoa fursa ya kipekee kwa wageni wanaotembelea ukanda wetu. |
|
|
photo by (code studio tanzania) |
| photo by (code studio tanzania) |
|
|
Looking forwards to see you at the 20th Sauti za Busara festival
Stone Town, Zanzibar, 9 - 12 February 2023
Karibuni nyote and welcome all. We promise the 20th edition will be extra special! |
|
|
Like and follow @sautizabusara |
| Busara Promotions P O Box 3635 Stone Town Zanzibar, Tanzania
[email protected]
Tel: +255 24 223 2423 or +255 773 822 294 |
|
|
Tafadhali sambaza kwa marafiki watakaopendezewa. Kujiunga au kujitoa kwenye jarida letu, andika barua pepe kwenda www.busaramusic.org |
|
|
|