Mwisho wa wito kwa wasanii: Sauti za Busara 2023
|
|
|
Usijibu kupitia barua pepe hii. Kwa kuwasiliana nasi tafadhali tuma kwa [email protected]
Unaweza kuwatumia ndugu na marafiki ikiwa wanapenda.
|
|
|
Sauti za Busara ni tamasha bora la muziki wa Afrika linalofanyika Mji Mkongwe, Zanzibar kila mwezi Februari, tamasha hili limefanikiwa kuvutia maelfu ya wadau wa muziki kutoka kila pembe ya dunia. Waanndaaji kwa sasa wapo katka harakati za maandalizi ya Tamasha la 20 litakaloanza tarehe 10th – 12th February 2023.
Hili litakuwa toleo maalum la kuadhimisha miongo miwili, na safu ya kusisimua ya wasanii, ushirikiano wa kisanii, mitandao ya kitaaluma, warsha za kiufundi na zaidi.
Sauti za Busara huonyesha muziki wa moja kwa moja ambao ni wa aina mbalimbali, wa kipekee na wenye utambulisho wa kitamaduni, nishati, msisimko na vibe chanya. Tamasha hili linatoa kipaumbele kwa wanamuziki wanawake, vijana na vipaji chipukizi kutoka katika bara zima la Afrika na viunga vyake..
Orodha ya wasanii watakao tumbuiza katika tamasha itatangazwa mapema mwezi Oktoba 2022.
|
Mwisho wa wito kwa wasanii
|
|
|
|
Tunawahimiza wasanii wote wanaocheza muziki wa kipekee uliounganishwa na Afrika, Ulimwengu wa Kiarabu au maeneo ya Bahari ya Hindi kutuma maombi ya kushiriki
Mwisho wa kupokea maombi yaliyokamilika ni tarehe 31 Julai 2022 (usiku)
Kwa taarifa zaidi na linki ya fomu ya maombi, tembelea https://www.busaramusic.org/call-for-artists-2023
Tafadhali hakikisha maombi yako yameambatanishwa wasifu wa msanii, nakala za kusikiliza (MP3) na video (MP4) ya onyesho lililofanywa mubashara, picha zenye ubora na au link ya kurasa yako ya Music in Africa. Jopo la uteuzi litapitia maombi yote yaliyokamilika na yaliyotumwa mpaka tarehe 31 July 2022.
|
|
|
Punguzo kubwa la tiketi litapatikana kuanzia tarehe 01 Julai, 2022 mtandaoni, likijumuisha bei maalum kwa watanzania, wenyeji wa Afrika Mashariki na wenye hati za kusafiria za Afrika.
|
|
|
Sauti za Busara 2022: Amplifying Women’s Voices
See video highlights from Sauti za Busara 2022, with Sampa The Great (Zambia), Sholo Mwamba (Tanzania), Sjava (South Africa), Ben Pol (Tanzania), Siti & The Band (Zanzibar), Msaki (South Africa), Vitali Maembe (Tanzania), Nadi Ikhwan Safaa (Zanzibar), Nomfusi (South Africa), Zan Ubuntu (Zanzibar), Fanie Fayar (Congo), Sylent Nqo (Zimbabwe), Wamwiduka Band (Tanzania), Suzan Kerunen (Uganda), Aleksand Saya (Reunion), Bahati Female Band (Tanzania) and more...
© CL Films & Busara Promotions, 2022
|
|
|
Kuanzia tarehe 19 - 23 Oktoba 2022, wajumbe wa WOMEX wataanza safari ya siku tano ya muziki katika jiji la kitamaduni na maridadi la Lisbon. Toleo la 28 kwa mara nyingine tena litawawezesha wataalamu wa biashara ya muziki duniani kuja pamoja, kushirikiana, kuungana, kuunda fursa mpya, na kushiriki maarifa muhimu na maarifa ya vitendo ili kukuza uchumi wa muziki duniani kote.
Jisajili mapema ili kupata ofa bora zaidi: www.womex.com
|
|
|
Music In Africa Foundation (MIAF) inafuraha kutangaza mkutano wa muziki wa ACCES toleo la 2022 utafanyika National Museum & House of Culture Theatre in Dar es Salaam tarehe 24, 25 na 26 Novemba. Tanzania itakuwa nchi ya tano barani Afrika kuwa mwenyeji wa ACCES, baada ya matoleo ya awali kufanyika nchini Senegal, Kenya, Ghana na Afrika Kusini.
"Tumekuwa tukitazamia kuandaa ACCES nchini Tanzania kwa muda," alisema mkurugenzi wa MIAF Eddie Hatitye. "Tuna furaha kubwa na tunatarajia toleo la kwanza kabisa la ACCES nchini Tanzania. Hii ni nchi ambapo muziki wa kitamaduni na wa kisasa unakusanyika ili kuunda eneo la muziki la kupendeza ambalo linastahili kusherehekewa na jukwaa la Kiafrika kama ACCES.Kwa taarifa zaidi, tembelea https://www.musicinafrica.net/acces
|
|
|
Tamasha la Sauti za Busara limekuwa likifanikishwa kwa msaada mkubwa kutoka taasisi mama ya Busara Promotions, kwa kuwezeshwa na Blue Amber Zanzibar. Blue Amber ni moja ya miradi ya kimkakati kwa Tanzania uliopo, Matemwe, pwani ya Kaskazini-Mashariki mwa, Zanzibar. Mradi huu mkubwa unaotarajiwa kuwa kivutio kikubwa cha mapumziko na burudani Afrika na kujulikana kama uwekezaji mkubwa wa kimkakati Tanzania
Tamasha bado linahitaji msaada mkubwa ilikuweza kufanikisha msimu wa kipekee wa 20. Manufaa mbalimbali ya udhamini na mwonekano unahakikishiwa kwa wafadhili wote, kwa pesa taslimu au aina tofauti ya ushiriki. Tafadhali wasiliana nasi ikiwa ungependa kushirikiana na Sauti za Busara 2023
|
|
|
|
Busara Promotions P O Box 3635 Stone Town Zanzibar, Tanzania
Find us off the airport road, Maisara
Tel: +255 242 232 423 or +255 773 822 294
|
|
|
Tafadhali shiriki jarida hili na marafiki ambao wanaweza kupendezwa. Kujiandikisha au kujiondoa kwa jarida letu, chapa tu barua pepe yako kwenye kisanduku katika tovuti www.busaramusic.org
|
|
|
|