Tangazo la orodha ya wasanii: Sauti za Busara 2023
|
Usijibu kupitia barua pepe hii. Kwa kuwasiliana nasi tafadhali tuma kwa [email protected]
|
Unaweza kuwatumia ndugu na marafiki ikiwa wanapenda.
|
|
|
Sauti za Busara, Stone Town, Zanzibar, 10 – 12 February 2023
Maudhui ya tamasha la 20 la Sauti za Busara ni Tofauti Zetu, Utajiri Wetu (Diversity is Our Wealth). Kuadhimisha muziki wa moja kwa moja kutoka barani Afrika na kwingineko, Tamasha huangazia wasanii wanawake, vijana na vipaji vinavyochipukia. Kuanzia Ijumaa 10 hadi Jumapili 12 Februari, Majukwaa mawili ndani ya Ngome Kongwe yatakuwa na maonyesho ya kusisimua na ya kipekee kutoka kwa
|
NNEKA (Nigeria), BCUC (South Africa), DAMIAN SOUL (Tanzania), MZEE WA BWAX (Tanzania), ASIA MADANI (Sudan / Egypt), PATRICIA HILLARY (Tanzania), CULTURE MUSICAL CLUB (Zanzibar), TARABBAND (Sweden / Iraq / Egypt), NAXX BITOTA (DRC / Canada), SANA CISSOKHO (Senegal), NASIBO (Zimbabwe), ZAWOSE REUNION (Tanzania), STONE TOWN ROCKERZ (Zanzibar), ZILY (Mayotte), ATSE TEWODROS PROJECT (Ethiopia / Italy), MAJESTAD NEGRA (Puerto Rico), UWARIDI FEMALE BAND (Zanzibar), KALOUBADYA (Reunion), OBERT DUBE (Zimbabwe), ZENJI BOY NA WENZAKE (Zanzibar), WAUNGWANA BAND (Zanzibar), SUPA KALULU (Zanzibar / Various) na wengine.
|
|
|
Tiketi za mapema zinapatikana hadi tarehe 31 Oktoba 2022, zikiwa na punguzo maalum kwa raia wote wa Tanzania, Wakazi wa Afrika Mashariki na wenye pasipoti za Afrika.
Tafadhali kununua Pasi za VIP ili kuonyesha mchango wako na ujipate T-Shirt ya ukumbusho!
Kwa bei za tiketi, vigezo na masharti, tembelea www.busaramusic.org/tickets.
|
|
|
In the picture from left to right (stand) Baraka Strato Moshi (Marketing Excutive: Fumba Town), Clara Werra (Head of Legal: Fumba Town) Verena Knippel & Julia Bishop (Busara Board Member) seat from left, Tobias Dietzold (CCO Fumba Town) Hon Simai M Said (Minister for Tourism and Antiquity) Yusuf Mahmoud, CEO Busara Promotions) at today’s Press Conference at Fumba Town.
|
|
|
|
Fumba Town Kushirikiana na Sauti za Busara
|
Fumba Town, mradi wa maendeleo ya kiikolojia wa CPS, imeingia makubaliano na Sauti za Busara kulipia gharama uendeshaji wa taasisi ya Busara Promotions kwa miaka mitatu. Ni mwendo wa dakika 20 tu kwa gari kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar, Fumba Town ndio mradi wa kwanza wa maendeleo endelevu Afrika Mashariki na inasifiwa kwa ubunifu ya kutengeneza majengo yenye ufanisi, yanayofikika katika soko la makazi.
|
|
|
"Tamasha hili limekuwa sehemu muhimu ya utamaduni wa Zanzibar kwa miaka mingi hivyo basi lazima sekta binafsi ichukue jukumu la kuunga mkono jitihadi hizi. Sauti za Busara huwaleta pamoja watu wa matabaka yote na kusisitiza umoja, amani na ustahimilivu katika jamii. Na hii ndio misingi ya Fumba Town na CPS na hivyo tunashukuru hupata nafasi ya kuchangia hili,” alisema Tobias Dietzold, Afisa Mkuu wa Biashara wa CPS.
"Tumejitolea kufanya tamasha la Sauti za Busara liwe imara na lenye nguvu kwa miaka ijayo huku tukifurahia utajiri na urithi wa tamaduni zetu mbalimbali kupitia muziki. Kupitia ushirikiano huu, tutahakikisha kwamba tunatoa mchango wetu mdogo, kwa miaka mitatu ijayo ili kuhakikisha tamasha linaendelea kuwepo kwa ustawi wa tamaduni,” aliongeza.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said alizipongeza Sauti za Busara na Fumba Town kwa kushirikiana pamoja ili kuendeleza na kusaidia ukuaji wa utalii visiwani humo.
"Kwa miaka 20 tamasha, limekuwa moja ya vivutio vikubwa kwa wageni katika kalenda yetu ya matukio ya kila mwaka. Tunatoa wito kwa mashirika yote ya serikali na viongozi, wafanyabiashara, makampuni binafsi, wahisani na wafadhili kuiga mfano mzuri wa CPS kuwekeza katika sanaa na urithi wetu wa kitamaduni ambao hunatoa kumbukumbu ya kipekee kwa wageni," alibainisha..
|
|
|
Mapato ya tiketi huchangia asilimia 30 ya gharama yote ya tamasha. Pamoja na kwamba gharama uendeshaji wa taasisi kwa kiasi kikubwa zinachangiwa na Fumba Town, tamasha bado linahitaji msaada wa wafadhili na washirika ili kuhakikisha linafanikiwa.
Fursa kwa wadhamini na wafanyabiasha za kutangaza biashara inapatikana
Kwa taarifa zaidi tembelea www.busaramusic.org/be-a-sponsor..
|
|
|
kupanga safari yako ya Zanzibar, tazama ukurasa wetu wa maelezo ya wageni kwenye www.busaramusic.org/travel.
Hapa utapata vidokezo muhimu kuhusu hoteli, visa na usafiri, chanjo, mahitaji ya afya na zaidi.
|
|
|
Mabanda na Wafanyabiashara
|
Tamasha linatoa fursa nzuri kwa wafanyabiashara kuonyesha bidhaa zao, kuuza vyakula na vinywaji, nguo, kazi za mikono na n.k. kwa maombi ya nafasi, tafadhali tuma barua pepe: [email protected]
|
|
|
Sauti za Busara huvutia watu kutoka kote ulimwenguni; wengi ni wataalamu wa tasnia ya muziki.
Movers & Shakers ni jukwaa letu la kila siku la wasanii wa ndani na nje ya nchi, mameneja, watangazaji, vyombo vya habari na wataalamu wengine kukutana na kubadilishana mawazo. Hakuna kiingilio, na nafasi ni chache. Kana utapenda kushiriki, tafadhali jiandikishe kupitia: https://www.busaramusic.org/movers-shakers/
|
|
|
Uidhinishaji kwa Vyombo vya Habari
|
Chumba maalum cha Waandishi wa Habari wa Tamasha na kupata kibali vya Picha au Filamu vinatolewa kwa wataalamu wanaotambulika pekee, wanaoliunga mkono au kulitangaza tamasha. Usajili wa mapema ni wa lazima; haiwezekani kusajili mlangoni.
Tafadhali jaza fomu ya usajili kupitia: www.busaramusic.org/press-accreditation
Kutuma linki mapema ya utangazaji wa tamasha kutasaidia maombi yako.
|
|
|
Kuanzia tarehe 19 - 23 Oktoba 2022, wajumbe wa WOMEX watakutana tena Lisbon, Ureno. Wataalamu wa kimataifa wa biashara ya muziki watakutana, watajadiliana, watatengeneza fursa mpya, na watapeana maarifa muhimu na ujuzi wa vitendo ili kukuza uchumi wa muziki duniani kote.
Taarifa zaidi: www.womex.com
|
|
|
|
Toleo la 5 la kongamano la Music In Africa’s ACCES litafanyika Dar es Salaam, Tanzania kuanzia tarehe 24 - 26 Novemba, kukiwa na mfululizo wa maonesho ya muziki, mikutano, mijadala ya wataalamu na mengineyo.
Atakaewahi kujisajili, ndie atakaepata nafasi ya kushiriki. Ni bure kwa wajumbe wa Kiafrika https://www.musicinafrica.net/acces
|
|
|
|
|
Busara Promotions P O Box 3635 Stone Town Zanzibar, Tanzania
Tunapatikana barabara ya uwanja wa ndege, Maisara
Tel: +255 242 232 423 au +255 773 822 294
|
|
|
Tufuatilie @sautizabusara
|
|
|
Tafadhali sambaza kwa marafiki watakao kupendezwa. Ili kujiandikisha au kujiondoa kwa jarida hili, andika anwani yako ya barua pepe kwenye kisanduku kilichopo www.busaramusic.org
|
|
|
|