Busara Logo

NEWSLETTER 

JAN 2023

Soma kwa  English / Kiswahili / français

Usijibu kupitia barua pepe hii. Kwa kuwasiliana nasi tafadhali tuma kwa [email protected], unaweza kuwatumia ndugu na marafiki ikiwa wanapenda.

Sauti za Busara 2023: Kuelekea tamasha la 20

  • Sauti za Busara 2023
  • Nunua Tiketi
  • Busara Plus @Fumba Town
  • Movers & Shakers
  • Washirika na Wafadhili
  • Maelezo ya Mgeni
  • Wasiliana na Busara
 

Artists Line-Up: Sauti za Busara 2023

ratio  
Tofauti zetu, Utajiri Wetu

Sauti za Busara, Stone Town, Zanzibar, 10 – 12 Feb 2023

Muda mchache umesalia kukaribisha toleo la 20 la tamasha maarufu duniani la Sauti za Busara. Kote Zanzibar na Tanzania, msisimko unaongezeka kwa shauku kubwa.

Februari 10 hadi 12, 2023, Sauti za Busara itaadhimisha miongo miwili iliyotumika kutafiti, kufufua na kutambulisha muziki wa asili ya Kiafrika kutoka kwa wakongwe wa tasnia hii, vipaji vipya, haswa kutoka kwa wanamuziki wa kike na bendi zinazoongozwa na wanawake, na sauti chache za thamani zilizosahaulika katika historia ya muziki. Punguzo kubwa la bei ya tiketi hutolewa kwa raia wa Tanzania, wakaazi wa EAC, na wote walio na pasipoti za Kiafrika.

Kaulimbiu ya toleo maalum la 20 la Sauti za Busara ni Tofauti Zetu, Utajiri Wetu (Diversity is Our Wealth). Kuadhimisha muziki wa moja kwa moja kutoka kote barani Afrika na kwingineko, kwa mara nyingine tena tamasha linaangazia wasanii wanawake, vijana na vipaji vinavyochipukia. 

Kuanzia Februari 10 - 12 February

TIKEN JAH FAKOLY (Côte d'Ivoire), BCUC (South Africa), DAMIAN SOUL (Tanzania), MZEE WA BWAX (Tanzania), ASIA MADANI (Sudan / Egypt), PATRICIA HILLARY (Tanzania), CULTURE MUSICAL CLUB (Zanzibar), NAXX BITOTA (DRC / Canada), SANA CISSOKHO (Senegal), NASIBO (Zimbabwe), ZAN UBUNTU (Zanzibar), ZAWOSE REUNION (Tanzania), STONE TOWN ROCKERZ (Zanzibar), ZILY (Mayotte), SWAHILI ENCOUNTERS (Zanzibar / Various), ATSE TEWODROS PROJECT (Ethiopia / Italy), MAJESTAD NEGRA (Puerto Rico), UWARIDI FEMALE BAND (Zanzibar), KALOUBADYA (Reunion), OBERT DUBE (Zimbabwe), ZENJI BOY NA WENZAKE (Zanzibar), WAUNGWANA BAND (Zanzibar), DCMA YOUNG STARS (Zanzibar), SUPA KALULU (Zanzibar / Various),KIKUNDI CHA IDARA YA UTAMADUNI (Zanzibar) na wengine wengi.

 

Nunua Tiketi

NUNUA TIKETI SASA

Tiketi za mapema zinapatikana hadi tarehe 31 Januari 2023,na viwango maalum kwa raia wote wa Tanzania, wakaazi wa Afrika Mashariki, na wamiliki wa pasipoti wa Kiafrika.

Tafadhali zingatia kununua Pasi za VIP ili kuchangia tamasha - na upate T-Shirt ya ukumbusho bila malipo!

Kwa bei za tiketi, sheria na masharti, ona www.busaramusic.org/tickets.

 

Busara Plus @Fumba Town

umba town logo
Busara-Plus-FINAL.jpg

Siku ya Jumamosi tarehe 11 Feb kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa kumi jioni, Fumba Town - mradi wa maendeleo ya kiikolojia wa CPS - ambao hivi karibuni waliungana na Sauti za Busara, watakuwa wenyeji wa Soko la Kwetu Kwenu ambapo mazao ya asili yaliyotengenezwa nchini, vyakula, nguo, kazi za mikono na Zaidi vitakuwepo. Tukio hili litakuwa na maonyesho ya bure kutoka kwa by Majestad Negra (Puerto Rico), Asia Madani (Sudan/Misri) na Siti & the Band (Zanzibar). Usafirishaji wa bure utapatikana kila nusu saa kutoka/hadi Ngome Kongwe.

Kwa maelezo zaidi na nyakati za utendaji, ona https://www.busaramusic.org/events/

 

Movers & Shakers

Women_in_Music_SzB2020_by_Link_Reuben
Movers_Shakers_SzB2019_photo_Link_Reuben

Sauti za Busara huvutia watu kutoka kote ulimwenguni; wengi ni wataalamu wa tasnia ya muziki.

Movers & Shakers ni jukwaa letu la kila siku la wasanii wa ndani na nje ya nchi, mameneja, watangazaji, vyombo vya habari na wataalamu wengine kukutana na kubadilishana mawazo. Hakuna kiingilio, na nafasi ni chache. Kana utapenda kushiriki, tafadhali jiandikishe kupitia

 https://www.busaramusic.org/movers-shakers/

 

Washirika na Wafadhili

Fumba-Town-and-CPS-Logo
CRDB Bank
ignite culture
acp
EU
HEVA
BC
SMZ
Ambassade de France à Dar es Salaam
Zanlink-Logo
institutfrancais
Australian-High-Commission-Kenya-stacked
kendwarocks
Serena Zanzibar
Emerson Zanzibar
Adventure_24_7
St-Bongo
mjini-fm-logo
COCONUT-FM
HODI-HODI-LOGO
DCMA
Alliance Francaise Dar
ZIFF
IOMMA LOGO
Music In Africa
2Tech Security
Afropop
AMPOLA
darlife
German Embassy Dar es Salaam

Fursa kwa wadhamini na wafanyabiasha za kutangaza biashara inapatikana

Kwa taarifa zaidi tembelea www.busaramusic.org/be-a-sponsor

 

Maalum Kwa Hoteli

Zimesalia siku chache kabla ya toleo la 20 la Sauti za Busara!

Kwa mchango wa USD 500 pekee, utajipatia tiketi 1 ya tamasha bila malipo kwa ajili yako au mmoja wa wageni wako uwapendao, au kuchangia USD 1,000 ili nembo yako ionyeshwe kwenye skrini kubwa kwenye tamasha na upokee tiketi 2 za bure.

Lipa hapa kupitia linki hii bila usumbufu: PesaPal Link

 
Accommodation artwork

Maelezo kwa Wageni

kupanga safari yako ya Zanzibar, tazama ukurasa wetu wa maelezo ya wageni kwenye www.busaramusic.org/travel.

Hapa utapata vidokezo muhimu kuhusu hoteli, visa na usafiri, chanjo, mahitaji ya afya na zaidi.

 

Wasiliana na Busara

Busara Promotions Logo

www.busaramusic.org
[email protected]

Busara Promotions
P O Box 3635
Stone Town
Zanzibar, Tanzania

Find us off the airport road, Maisara
Tel: +255 242 232 423 or +255 773 822 294

Tufuatilie @sautizabusara

Facebook Twitter Instagram YouTube Flickr

Tafadhali sambaza kwa marafiki watakao kupendezwa. Ili kujiandikisha au kujiondoa kwa jarida hili, andika anwani yako ya barua pepe kwenye kisanduku kilichopo www.busaramusic.org