Press Kiswahili

  • This mailing list is a public mailing list - anyone may join or leave, at any time.
  • This mailing list is announce-only.

Orodha hii ya kutuma barua imekusudiwa tu kueneza habari zinazohusu Tamasha la Sauti za Busara kwa vituo au vyombo vya habari

Privacy Policy:

Sera faragha ya, Busara Promotions Press : Barua pepe zote katika orodha hii itatumika kwa madhumuni ya kukujuza shughuli zote zinazoendelea Busara Promotions. Hazitatolewa wala kupewa mtu mwingine au taasisi yeyote.

Archived Messages

 

Press Kiswahili Message

February 14th 2023 MST

Tamasha la Sauti za Busara 2023 lahitimishwa kibabe, tarehe ya tamasha la 2024 yatajwa Taarifa kwa Vyombo vya Habari Februari 14, 2023 Zanzibar. Tamasha la 20 la Sauti za Busara linalosifika kimataifa lilifikia katika kilele cha kusisimua Jumapili usiku baada ya siku tatu za burudani ya nguvu zilizoing’arisha Ngome Kongwe na vitongoji vya Mji wa Stone Town. Tamasha la 2023 lilifanyika chini ya kauli mbiu: “Utofauti Wetu, Utajiri Wetu.” Katika maelezo yake, mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud ali ...Continue Reading

Press Kiswahili Message

February 10th 2023 MST

Sauti za Busara kuanza leo na vipaji vya nyumbani Taarifa kwa Vyombo vya Habari Februari 10, 2023 Unguja. Baada ya miaka 19 ya mafanikio, Sauti za Busara, moja ya matamasha bora barani Afrika, leo Ijumaa Februari 10 katika eneo la Ngome Kongwe, Stone Town, Sauti za Busara itashuhudia toleo la 20 tangu kuanzishwa kwake.  Kikundi cha DCMA Young Stars, ambao ni watoto wadogo wenye vipaji kutoka shule tofauti visiwani Zanzibar litalinatarajia kutumbuiza na wanamuziki na walimu kutoka Chuo cha Muziki cha Dhow Count ...Continue Reading

Press Kiswahili Message

February 8th 2023 MST

** *TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI* */Februari 8, 2023/* *Kwa nini **Sauti za Busara linaendelea kuwa tamasha la kipekee* *Unguja*. Tamasha la Sauti za Busara la 20 linatarajiwa kuanza Ijumaa, Februari 10, ambapo Stone Town na viunga vyake vitalibeba tamasha hili la burudani ya muziki wa Kiafrika kwa siku tatu mfululizo ndani ya Ngome Kongwe. Kuna shughuli mbalimbali zinazoendelea katika eneo hilo la kihistoria huku maelfu ya tiketi zikiwa tayari zimeshauzwa kwa wageni wanaotoka katika kila pembe ya dunia. “Miaka 2 ...Continue Reading

Press Kiswahili Message

January 31st 2023 MST

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI* */31 Januari 2023/* *Sauti za Busara baada ya Miaka 20 ni Hadithi ya Enzi* Toleo la 20 la tamasha la Sauti za Busara linatarajiwa kutikisa kuta za Ngome Kongwe huko Zanzibar (Ngome Kongwe) kwa siku tatu kuanzia tarehe 10 hadi 12 Februari. Iinasifiwa kimataifa kama moja ya tamasha kuu za muziki barani Afrika, mwaka huu inaadhimisha miaka ishirini ya kuonyesha muziki bora wa Kiafrika, hatua muhimu ambayo matamasha mengine machache katika Bara la Afrika yamefikia. Licha ya changamoto n ...Continue Reading

Sauti za Busara 2023: Kuelekea tamasha la 20

January 23rd 2023 MST

NEWSLETTER  JAN 2023 Soma kwa  English / Kiswahili / français Usijibu kupitia barua pepe hii. Kwa kuwasiliana nasi tafadhali tuma kwa busara@PROTECTED, unaweza kuwatumia ndugu na marafiki ikiwa wanapenda. Sauti za Busara 2023: Kuelekea tamasha la 20 Sauti za Busara 2023 Nunua Tiketi Busara Plus @Fumba Town [*]Movers & Shakers Washirika na Wafadhili Maelezo ya Mgeni [*]Wasiliana na Busara Artists Line-Up: Sauti za Busara 2023 Sauti za Busara, Stone Town, Zanzibar, 10 – 12 Feb 2023 Muda mchache ...Continue Reading

Press Kiswahili Message

November 21st 2022 MST

PRESS RELEASE for publication 21 Nov 2022 Sauti za Busara yazindua orodha ya nguvu ya wasanii kusheherekea miaka 20 Zanzibar. Waandaji wa Tamasha maarufu la muziki wa Kiafrika la Sauti za Busara ambalo hufanyika Mji Mkongwe, Zanzibar kila Februari, wametangaza orodha ya wasanii itakayolifanya toleo la ishirini la mwaka wa 2023 liwe la kukumbukwa. Likishirikisha bendi maarufu na zinazochipukia kutoka kanda zote za Bara la Afrika, likiongozwa na msanii nguli wa muziki wa reggae barani Afrika Tiken Jah Fakoly, kuto ...Continue Reading

Press Kiswahili Message

March 23rd 2022 MST

  Baada ya miaka 19 ya kusherehekea tamaduni tofauti na muziki wa Kiafrika, pazia la Sauti za Busara linafungwa   Zanzibar: Kwa huzuni na masikitiko makubwa, Busara Promotions inatangaza kusitisha shughuli zake ifikapo tarehe 31 Machi 2022, kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha. Bila fedha za kulipa gharama za ofisi au mishahara, haiwezekani tena kwa taasisi inayosifika kimataifa kuendelea. Tangu kusajiliwa kwake Zanzibar mnamo Machi ...Continue Reading

Press Kiswahili Message

February 15th 2022 MST

*Taarifa kwa vyombo vya Habari* *Februari 14, 2022* *Sauti za Busara lahitimishwa huku Serikali ikiahidi kulisaidia tamasha hilo* *Zanzibar*. Tamasha la 19 lenye hadhi ya kimataifa linalofahamika kwa jina la Sauti za Busara lilifikia kikomo usiku wa Jumapili baada ya burudani ya nguvu ya siku tatu ambalo lilifanyika katika eneo la Ngome Kongwe, Stone Town. Tamasha la 2022 lilifanyika chini ya Kauli mbiu: ‘Paza Sauti’. Katika hotuba yake ya ufunguzi, mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud alibainisha kwamba kat ...Continue Reading

Press Kiswahili Message

February 9th 2022 MST

*Taarifa kwa vyombo vya habari* *Februari 11, 2022* *Sauti za Busara 2022 inaanza leo* *Zanzibar.* Sauti za Busara, moja ya tamasha zinazoongoza barani Afrika, inaanza leo Ngome Kongwe, Stone Town huku wasanii mbalimbali kutoka Tanzania na sehemu nyingine za Afrika wakitarajia kutumbuiza mubashara. Mbali na vikundi vinne vilivyo wahi kutumbuiza katika tamasha hilo, vingine vyote vinashiriki tamasha hilo kwa mara ya kwanza. Akizungumza mjini Zanzibar siku ya Alhamisi, Mkurugenzi wa tamasha hilo Yusuf Mahmoud amewata ...Continue Reading

Press Kiswahili Message

January 31st 2022 MST

*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI* *Tamasha la Sauti za Busara kuendelea kuteka hisia* *Zanzibar, Februari 1:* Tamasha la Sauti za Busara litarindima tena Mji Mkongwe, Zanzibar kuanzia Februari 11 hadi 13 huku likiwa na kauli mbiu ya ‘Tunakomaa!’. Mwaka 2020 na 2021 haikuwa miaka mizuri kwa wasanii, wabunifu na utalii wa kitamaduni kulingana na changamoto ulioletwa Uviko-19. Sauti za Busara kwa sasa huenda ndiyo tamasha pekee lenye uzoefu wa muziki unaofanyika mubashara wa Kiafrika ambalo hufanyika kila mwaka, linal ...Continue Reading