Shukrani za dhati kwa kila mmoja aliyeshiriki nasi kwa tamasha la 22 la Sauti za Busara 2025, Bila ninyi tusingefanikiwa! kwapamoja, tulicheza, tulimba, tulisherehekea, na tulitengeneza kumbukumbu nzuri hadi mwisho wa tamasha.
Upendo wenu, na shauku yenu zilifanya toleo la 22 kuwa lenye mafanikio makubwa, na tunashukuru sana kuwa nanyi kama sehemu ya familia yetu. Tunapomaliza tamasha la mwaka huu, tunasema ASANTE SANA kutoka kwenye mioyo yetu. Kauli mbiu “Voices for peace” iliguswa sana kupitia tamasha hili, na tunatumai itabaki katika nyoyo zetu daima, ikitufundisha kueneza ujumbe wake popote tutakapokwenda. Amani itufungue kwenye kila tunalofanya, mpaka tutakapokutana tena.
Tunakusubiri tena kufanya yote haya mwaka kesho, Yajayo ni mazuri zaidi!
Tutaonana 2026!
Ili kupata ladha kidogo ya kile kilichojiri katika tamasha Sauti za Busara 2025 tafadhali tazama viungo vilivyo hapa chini!