FuTopia inaandaliwa na Busara Promotions kwa ushirikiano na Fumba Town, FuTopia si tu tamasha bali ni jukwaa la harakati. Ni sherehe hai, inayokua, na kutoa nafasi katika Nyanja ya ubunifu, ujumuishaji, jamii na furaha. Kadiri inavyokua, FuTopia inakusudia kuwa moja ya Tamasha kubwa na lenye kuvutia zaidi katika Afrika Mashariki, ikiwawezesha na kufanikisha shughuli za ubunifu kustawi.
FuTopia inaweza kuwa mpya, lakini msingi wake umejikita na Inaakisi dhamira kuu ya Busara Promotions ya kuwawezesha wasanii katika Nyanja tofauti kupata masoko ya kazi zao na kuwa huru katika ufanyaji wa shughuli zao, kujenga majukwaa endelevu kwa vipaji na wataalamu wa Kiafrika, na kukuza uhusiano na ushirikiano.
Karibu FuTopia — Karibu katika jukwaa la sanaa inayoishi!