Newsletter Oct 2020 Sauti za Busara 2021: English / Swahili / français Usijibu kupitia barua pepe hii. Wasiliana nasi kupitia [email protected] Tafadhali wajulishe na wenzio watakaopendezwa na jarida hili Kila mwaka mnamo mwezi wa pili, Sauti za Busara Zanzibar inawakutanisha watu kutoka bara la Afrika na kwingineko kusheherekea muziki halisi wa Afrika. Kama kawaida toleo la 18 litatikisa kuta za Mji Mkongwe kwa tarehe 12 na 13 Februari 2021. Tutahakikisha tunatoa kipaumbele vya usalama, afya na mali za wasanii, wageni na wenyeji. Tamasha hili linaandaliwa na Busara Promotions, taasisi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa hapa Zanzibar. Morena Leraba, Lesotho Yugen Blakrok, South Africa Dogo Fara, Reunion Tofa Boy, Zanzibar Siti Muharam, Zanzibar Sika Kokoo Band, Ghana Barnaba Classic, Tanzania Maallem Abdelkebir Merchane, Morocco Sandra Nankoma, Uganda #SzB2021 Festival Line-upYugen Blakrok (South Africa); Milton Gulli (Mozambique); Barnaba Classic (Tanzania); Siti Muharam (Zanzibar); Dawda Jobarteh (The Gambia); Maallem Abdelkebir Merchane (Morocco); Djam (Algeria); Morena Leraba (Lesotho); Sika Kokoo (Ghana); Sandra Nankoma (Uganda); Dogo Fara (Reunion); Tofa Boy (Zanzibar); Misoji Nkwabi (Tanzania); Shabo Makota (Tanzania); Stone Town Rockerz (Zanzibar / Tanzania); ...and morena wengineo watakapoendelea kuthibitisha ushiriki wao. Orodha ya Wasanii Kwa kuwajua zaidi, angalia video zao na soma taarifa zao kupitia tovuti yetu. Tiketi & Pasi Tiketi za tamasha la Sauti za Busara 2021 zinapatikana mtandaoni kupitia tovuti yetu kwa uhakika na usalama zaidi, pata punguzo maalum kwa watanzania, kwa wenye vibali vya kuishi Afrika mashariki, na wote watakao nunua mapema kabla ya tarehe 31 Oktoba. Kwa kujua bei na kununua tiketi bofya link www.busaramusic.org/festivals/tickets/ Taarifa kwa wageni Kama ni mara yako ya kwanza kufika Zanzibar pitia linki kwa ajiri ya taarifa mbalimbali Info for Visitors
Jihusishe na Tamasha: kuwa muwezeshaji wa Tamasha Tamasha linawatangaza wadhamini wake wote kwenye machapisho yake kama mabango kwenye ukumbi wa tamasha, mkutano wa waandishi wa habari na mitandao ya kijamii Youtube, facebook, Instagram, na twitter.
Sponsor * Be a Friend of Busara Kwa watakao hitaji kuwa wadhamini wa tamasha wawasiliane na Meneja wa tamasha [email protected] Shukrani kwa wadhamini wetu, wachangiaji na washirika kwa kulisaidia tamasha la Sauti za Busara 2021
Vyomba vya Habari Kwa wale wote watakao hitaji kuomba vitambulisho vya waandishi wa habali mwisho wa maombi ni tare 2/1/2021
Usajili wa mapema ni lazima kwa wana habari wote; haitawezekana kuomba ukumbini. Kuna aina tatu za vitambulisho vya mikutano: kitambulisho cha kwenye chumba cha mahojiano tu, kitambulisho cha kupiga picha tu, kitambulisho cha mchukua video. Tafadhali omba kitambulisho ambacho ni sahihi kwako, kumbuka nafasi ni chache kwa waombaji, kwa hiyo si wote watakaopata vibali.
Kwa maelekezo zaidi kuhusu vibali vya wana habari bofya hapa.
Wafanyabiashara Idadi ni chache kwa watakaohitaji nafasi yakufanya na au kutangaza biashara zao ndani ya tamasha. Vipaumbele vinatolewa kwa wafanyabiashara wa Afrika Mashariki wenye bidhaa tofauti kama wachongaji, wachoraji, wauza vyakula, nguo, muziki na viburudisho. Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia barua pepe [email protected]
Matukio mengine #SOULIDARITY Campaign JE, wewe ni msanii wa Afrika uliyepoteza nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha kutokana na virusi vya Korona? Kampeni ya #SOULIDARITY ipo kwa ajili ya kukusaidia. Jisajili na jiunge nao kupitia www.soulidarity.org Wasaidie wanamuziki wa Afrika na sambaza ujumbe wa kampeni hii kwa watu wengine. Kila mtu afanye awezalo ili muziki lazima uendelee. www.soulidarity.org Marafiki Festival 8 – 9 Oktoba: The Slow Leopard, Dar es Salaam 10 Oktoba: Firefly, Bagamoyo Tamasha litashirikisha waasanii na bendi mbalimbali kutoka Tanzania kama Sikinde, Msafiri Zawose, Siti & the Band, Rich Lumambo, Malfred, Wamwiduka Band, Misoji Nkwabi, Abeneko & Positive Mind, Ze Spirits, Afro Simba, Shabo Makota na wengine wengi Jambiani Vibes Tarehe 10 Oktoba, kuanzia saa nne Asubuhi hadi saa nne usiku, katika ufukwe wa New Tedd’s Jambiani, Zanzibar. Kutakuwa na masaa 12 ya muziki kutoka kwa Malfred, Ras Coco, Wakushi Band, Taffa na the band, Willa the Note na wengine wengi. Warsha, vyakula, vinywaji na michezo mingine mingi kwa familia. https://www.teddys-place.com/ WOMEX (World Music Expo) Kwa mara ya kwanza WOMEX kufanyika mtandaoni kuanzia tarehe 21 – 25 Oktoba. Toleo hili la mtandaoni litaruhusu majadiliano, mazungumzo na muziki kuendelea, na muingiliano wa kudunia kubaki kuwa imara zaidi.
Kwa taarifa zaidi na kujisajili: https://www.womex.com/virtual/piranha_arts_1/news/womex_20_digital_1 Wasiliana nasi Busara Promotions Find us off the airport road, Maisara Tel: +255 24 223 2423 Tafadhali unaweza kushea na marafiki zako watakao penda jarida hili. Kujisajili kwa ajili ya majarida yetu andika barua pepe pepe yako katika kiboksi kupitia www.busaramusic.org
|