Muziki wa Afrika wachangamsha Zanzibar, 100% Mubashara! Soma jarida kwa Kingereza / Kiswahili / Kifaransa
Usijibu kupitia anwani hii . Kwa mawasiliano tafadhali tumia [email protected] Unaweza kusambaza kwa marafiki ambao wanapenda kujihusisha. Vitali Maembe (Tanzania) audience at Sauti za Busara 2021 (photo Link Reuben) Msafiri Zawose (Tanzania) audience at Sauti za Busara 2021 (photo Link Reuben) Vitali Maembe (Tanzania) audience at Sauti za Busara 2021 (photo Link Reuben) Sauti za Busara 2021 audience (photo Lorenzo Maccotta) Siti Muharam (Zanzibar) at Sauti za Busara 2021 (photo Marc Ngotonie) Dulla Makabila (Tanzania) at Sauti za Busara 2021 photo by Link Reuben Barnaba Classic (Tanzania) at Sauti za Busara 2021 photo by Marc Ngotonie Tarajazz (Zanzibar) at Sauti za Busara 2021 photo by Marc Ngotonie Stone Town Rockerz (Zanzibar) at Sauti za Busara 2021 (photo Link Reuben) Morena Leraba (Lesotho) at Sauti za Busara 2021 (photo Link Reuben) Ison Mistari aka Zenji Boy (Zanzibar) at Sauti za Busara 2021 (photo Link Reuben) Msafiri Zawose (Tanzania) at Sauti za Busara 2021 (photo Link Reuben) Shabo Makota (Tanzania) at Sauti za Busara 2021 (photo Marc Ngotonie) Vitali Maembe (Tanzania) at Sauti za Busara 2021 (photo Link Reuben) Djam (Algeria) at Sauti za Busara 2021 (photo Marc Ngotonie) Sandra Nankoma (Uganda) at Sauti za Busara 2021 (photo Marc Ngotonie) Sauti za Busara 2021 Tamasha la Sauti za Busara 2021 lilifanyika Ngome Kongwe, Zanzibar Tarehe 12 – 13 Februari, ikishuhudia programu ya muziki mubashara kutoka Zanzibar, Tanzania, Uganda, Lesotho na Algeria.
Wasanii chipukizi na wale wachanga walitia fora ni pamoja na Dulla Makabila, Tanzania;Sandra Nankoma, Uganda; Morena Leraba, Lesotho; TaraJazz, Zanzibar; Stone Town Rockerz, Zanzibar; Siti Muharam, Zanzibar; Shabo Makota, Tanzania; Zenji Boy, Zanzibar; Richie Lumambo, Tanzania; Tofa Boy, Zanzibar, Hawa walitumbuiza kwenye jukwaa moja na magwiji kama Vitali Maembe, Tanzania; Msafiri Zawose, Tanzania; Djam, Algeria na Barnaba Classic, Tanzania.
Kwa miaka mingi iliopita tumekuwa tukijuiliza kama kuna maana ya kuendelea na tamasha hili Lakini kwa mara nyingine maudhurio ya zaidi watu 3000 yamedhihirisha kwamba tamasha lina umhimu wake .
Hakuna sehemu yoyote ya ulimwengu ambayo haina virusi vya korona, lakini watu wa Tanzania wamepata njia za kuishi nayo. Ali Juma, mfanyabiashara mwenye banda ndani ya Ngome Kongwe alisema virusi vya korona sio vya kuondoka hivi karibuni kwa hiyo ni muhimu kujifunza kuishi navyo huku tukichukuwa taadhari kama wanavyo shauri wataalam
Wasanii nao walitoa hisia kama hizo wakati wa kutumbuiza na hata baada huku wakisisitiza kwamba maisha yao yanategemea majukwaa. Kutokana vizuizi vya kusafiri vilivyoweka na nchi nyingi tamasha liliamua kwenda na vipaji kutoka Tanzania. Tunashukuru wadhamini, wahisani na washirika wetu kwenye tasnia ya habari kama Plus TV waliorusha mubashara tamasha nzima kwenye DStv channeli 294. Media Coverage Sauti za Busara 2021: 2,500 Gather to Celebrate Music Unlocked By The Arts Desk, 19 Feb 2021 “Although there were clearly some overseas visitors, travel restrictions meant the international numbers were down, which is why the stream on Plus TV was put in place to keep in touch with audiences across Africa and beyond. As so often, the pandemic has led to innovations that will probably stay in place once the virus has passed”…read more Sauti za Busara 2021: Organisers pull off successful fest amid challenging times By Music in Africa, 17 Feb 2021 East Africa’s favourite festival Sauti za Busara was held at the historic Old Fort in Stonetown, Zanzibar, on 12 and 13 February. It brought together artists from South Africa, Algeria, Uganda and Tanzania for a weekend of eclectic performances under the theme, Alive & Kickin …read more Messages of hope as Sauti za Busara reaches climax The Citizen, 15 February 2021 The 18th edition of the Sauti za Busara came to hilarious climax on Saturday night after two days of performances that brought life to the Old Fort and Stone Town. Featuring an array of artistes who were performing for the first time on the iconic stage, the festival brought back distant memories of pre-pandemic years when the setting was a melting point of African culture. Singeli artist Dullah Makabila was a special attraction as he got the audience dancing to the final climax … read more See more media highlights at www.busaramusic.org/media-coverage See photo highlights at www.flickr.com/photos/sautizabusara
Mazingira Yetu, Maisha Yetu Kampeni ya Sauti za Busara 2021 ilikuwa ni ‘MazingiraYetu, MaishaYetu’ (Our Environment, Our Life).
Mradi huu uliangazia kuongeza uelewa, kutangaza mazungumzo na matendo ya kusaidia mazingira. Matukio yaliangazia matumizi endelevu ya vifaa vya plastiki na hatari plastiki zinazotumika kwa mara moja (single use) mazingira ya bahari, uvuvi usiofaa, kukata miti hovyo na mengineyo.
Katika kuelekea kipindi cha Tamasha, Busara imeshirikiana na taasisi nyingine ‘The Creative Education Foundation Zanzibar’ shule ya watoto yatima na wenye mazingira magumu ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu ya mazingira moja kwa moja.
Wanafunzi arobaini walifanya safari ya kwenda kisiwa cha Chumbe ambapo waliweza kujifunza jinsi ya kuvuna maji ya mvua, uhifadhi wa maji, utengenezaji wa mbolea asili na bustani enedelevu. Darasani walisoma kuhusu matumbawe na samaki, na kupata fursa ya kutembelea miti ya mikoko na jinsi ya utunzaji wa kisiwa. Majadiliano ya athari za plastiki ikafuatiwa na shughuli za uzamiaji kwa ukaribu zaidi ili kurahisisha uelewa na viumbe vya baharini.
Baada ya safari ya siku, wanafunzi waliweza kuandaa michoro yenye ujumbe wa ‘MazingiraYetu, MaishaYetu’ na kufanya maonyesho Mji Mkongwe kwenye jengo la Hifadhi Zanzibar. notes in the mangroves marine conservaton from below By Farida, 15 yrs Village Life - Salum, 15 yrs The Beach - Saidi, 14 yrs Tuzo ya Emerson Foundation Hongera kwa Khamis Maulid Mwita, kwa kujishindia tuzo ya Emerson Zanzibar Foundation Music Award 2021, Mwita alipata shilingi 2,000,000 TZS, pamoja na cheti. Kauli mbiu yam waka huu ni ‘Old is Gold’, iliyokuwa na lengo la kuhamasisha waimbaji wapya wa taarab ya asili. Majaji waliwapongeza washiriki wote kwa ushindani waliouonyesha.
EZF inaendelea kusaidia wasanii vijana na wenye vipaji kwa kuwapatia fursa na kutambulika. Inazidi kuonyesha na kuangazia maono ya marehemu Emerson D. Skeens, ambaye ni mwanzilishi wa Zanzibar International Film Festival, Dhow Countries Music Academy na Sauti za Busara. Lengo kuu la Emerson lilikuwa kuwasaidia wenyeji, na vilevile aliweza kuanzisha Hoteli maarufu Emerson Spice and Emerson on Hurumzi. Busara Xtra EZF Music Award at Sauti za Busara 2021 (photo Marc Ngotonie) Shukrani kwa Wadhamini na washirika Shukrani zetu za dhati ziende kwa wawezeshaji wetu akiwemo CRDB Bank, SerikaliyaMapinduziya Zanzibar, Zanlink, Emerson Zanzibar, ZIFF, Plus TV, Chuchu FM, ZBC, Zanzibar Cable TV, Music In Africa, Pili Pili Hotels, Firefly Bagamoyo, 2Tech Security, Coastal Aviation, DCMA Zanzibar, Tasakhtaa Hospital, ZESS, Golden Tulip Dar City Centre, La Taverna Restaurant, Café Foro, Stone Town Café, Zanzibar Serena Hotel, Mozeti Tours & Safaris, Azam Marine, Colors of Zanzibar, Swahili Soft Technologies, United Petroleum, ZANREC, Dar Life na wengineo.
Busara Promotions Find us off the airport road, Maisara Tel: +255 24 223 2423 Please share this mail with friends who may be interested. To subscribe or unsubscribe to our newsletter, simply type your email address in the box at www.busaramusic.org |