Kwanza kabisa, tungependa kutoa shukrani nyingi kwa wapenzi wote wa muziki, wasanii, wafanyakazi na wafuasi ambao wamefanya Toleo la 21 kuwa toleo jingine la kuwekwa katika kitabu cha historia .Lilikuwa tamasha la kuvutia na kusisimua wikendi nzima.
Kwa muda wa siku tatu, takriban watu 20,000 kutoka duniani kote walihudhuria na kushuhudia utajiri na utofauti wa wasanii wa tamasha hilo, wakifurahia gwaride la tamasha lililorudi baada ya mapumziko ya COVID, pamoja na majukwaa mawili vya bure; Moja katika bustani ya Forodhani na jukwaa jingine katika Mji wa Fumba.
Tamasha la mwaka huu lilionyesha na kusheheni vipaji vya kiwango cha kimataifa kutoka Nigeria, Afrika Kusini, Msumbiji, Zanzibar na Tanzania, Kenya, Algeria, Uganda, Zimbabwe, DRC, Reunion na Ethiopia.
Ili kupata ladha kidogo ya kile kilichojiri Sauti za Busara 2024 tafadhali tazama viungo vilivyo hapa chini!