Toleo la 22 la Sauti za Busara mwaka huu, lenye mada ya Amani na Umoja, linasherehekea muziki wa moja kwa moja kutoka Afrika, pamoja na talanta mpya na zinazoibuka. Tamasha hili linakusanya bendi maarufu na zinazoibuka kutoka kila kona ya bara la Afrika, likiongozwa na wasanii wakuu kama Thandiswa (South Africa), Blinky Bill (Kenya), Christian Bella & Malaika Band (Tanzania), Bokani Dyer (South Africa), Frida Amani (Tanzania), Wura Samba (Nigeria), The Zawose Queens (TZ/UK), Kasiva Mutua (Kenya), Zanzibar Taarab Heritage Ensemble (Zanzibar), Leo Mkanyia & Swahili Blues (Tanzania, Boukouru (Rwanda), Tryphon Evarist (Zanzibar, Charles Obina (Uganda), Baba Kash (Tanzania) Anna Kattoa & Bantu Sound (Zanzibar).
Wasanii wengine watakaoshiriki ni Tarabband (Sweden), Assa Matusse (Mozambique), Mumba Yachi (Congo), Nidhal Yahyaoui (Tunisia) ), Étinsel Maloya (Reunion), WD Abo (Sudan), B.Junior (Mayotte), uKhoiKhoi (South Africa), Joyce Babatunde (Cameroon) na wengine zaidi!