Salamu za Desemba 2024

Mádé Kuti & The Movement (Nigeria)

Shukrani za Dhati

Familia ya Sauti za Busara,

Mwaka unapokaribia kumalizika, tunakumbuka kwa furaha na shukrani namna tuliyoshirikiana pamoja katika tamasha la Sauti za Busara. Kila tamasha lililopita mlifanya kuwa moja ya tamasha bora na maarufu la muziki, utamaduni, na umoja. shukrani sana kwa maonesho yote kutoka kwa wasanii, umati wa mashabiki zetu, na hamasa na chachu ya kuzidi kuendelea kuwapa burudani ya kweli ya muziki wa kiafrika.

Mwaka wa 2024 ulikuwa wa kipekee, na Tamasha la kuvutia kutoka kwa wasanii wa ndani na kimataifa waliojitokeza kwenye jukwaa letu. Mapigo ya muziki, rhythm, na hadithi tulizoshiriki zilisikika kwa muda mrefu baada ya tamasha kumalizika. Hatuna maneno ya kutosha kuwashukuru kwa kuwa sehemu ya safari hii ya kuvutia, na tayari tunajiandaa kufanya mwaka wa 2025 kuwa wa kipekee zaidi!

Jiandaa kwa Sauti za Busara 2025: Tamasha la Muziki la Mwaka!

Tunafurahi na tunasubiri kwa hamu kwa ajili ya lineup ya wasanii wa mwaka 2025, ambayo inahakikisha kuwa itakuwa yenye kuvutiana isiosahaulika.

Sauti za Busara 2025 Line-Up

Sauti za Busara 14 - 16 February 2025:

Voices for Peace

Sauti za Busara inarudi kwa ukubwa, bora, na utofauti zaidi kuliko ilivyokuwa kabla! Kuanzia tarehe 14 hadi 16 Februari 2025, tutawaunganisha wanamuziki kutoka kila kona ya dunia ili kusherehekea utajiri na uzuri wa muziki na tamaduni za Kiafrika. Tamasha hili la kipekee litafanyika katika mandhari ya kuvutia ya Stone Town, Zanzibar, na linahakikishia kuwa itakuwa ni sherehe isiyosahaulika ya sauti, umoja, na nguvu ya muziki kwa amani.

Sauti za Busara 2025 Advance Tickets

Tiketi za Mapema: Epuka Foleni!

Tunajua kuwa kusubiri kwenye foleni si jambo la kufurahisha kwa mtu yeyote, kwa hivyo kwanini usiepuke hilo? 

Ili kufanya ufurahie zaidi, nunua tiketi yako ya mapema sasa! Kwa kununua tiketi zako mapema, hutapoteza muda na,  pia utapata bei nafuu! Usisubiri hadi dakika ya mwisho, epuka foleni na kwa kujipatia tiketi sasa

Tiketi za Mapema Zinatolea:

Upendeleo wa kuingia kwenye lango la tamasha kwa kuepuka foleni ndefu!

Bei za punguzo unaponunua mapema!

Nunua sasa kupitia Tukiio au tovuti yetu na tuufanye mwaka wa 2025 kuwa usiosahaulika!

Tunasubiri kwa hamu kukuona tena kwenye Tamasha la Sauti za Busara 2025. Endelea Kutufuatilia kupitia kwenye mitandao ya kijamii, jiandikishe kwa jarida letu, na kuperuzi kwenye tovuti yetu kwa taarifa zaidi kuhusu wasanii, bei za tiketi, na ratiba za tamasha.

Nunua Tiketi Hapa!
Francesco Nchikala (DRC) at Sauti za Busara 2024
Festival Goers at Sauti za Busara 2024 (Markus Meissl)
The Brother Moves On (South Africa) at Sauti za Busara 2024
Kenya Airways Discount on Travel

Punguzo la bei kwa Ndege zote za Kenya Airways kwenda Zanzibar

Tunafurahi kutangaza msimbo(Code) wa ofa rasmi kutoka kwa washirika wetu wa ndege, Kenya Airways, kwa Sauti za Busara 2025! Pata punguzo la kipekee la 20% kwa kutumia msimbo (Code) wa ofa SAUTI25 unapohifadhi au kununua tiketi zako za ndege na Kenya Airways.


Safari za anga ndani ya Afrika, na kuadhimisha muziki wa kiafrika! Tutaonana mwezi Februari!

Tumia msimbo(Code) wa ofa: SAUTI25


Punguzo: 20% kwa madaraja yote ya Economy na Business 

Muda wa Mauzo: Hadi Februari 10, 2025.
Muda wa Safari: Februari 7, 2025 - Februari 23, 2025.
Inatumika kwa Safari za Kurudi tu(Return Tickets).
Inatumika kwa ndege zote za KQ zinazofanya safari kwenda Zanzibar.

Agiza safari yako hapa!
Happy Holidays!
Happpy Holidays from Busara

Kutoka Team ya Sauti za Busara, tunakutakia mwaka mpya wenye furaha, amani, na mafanikio. Asante, na tunatarajia kuwa na wewe hivi karibuni!

Kheri ya mwaka mpya

Team Busara

#SzB2025 #VoicesforPeace #IgniteYourStory #AmaniNdiyoMpangoMzima

Fumba Town Logo
Clouds Media Group
Kenya Airways
French Embassy Tanzania
Littlegig
Zanlink Logo (without LT) CMYK copy-1.png
Volks.House
Sauti za Busara - One Africa

Follow us on Social Media to get the latest updates:

This e-mail has been sent to [[EMAIL_TO]], click here to unsubscribe.

Busara Promotions. Maisara, Stone Town 3635 Zanzibar City TZ