Hisi midundo. Furahia msisimko
Sauti za Busara linarejea tena Zanzibar,05 - 08 Februari,2026 na tunaanza kwa kuzindua rasmi tiketi za mapema kwa punguzo maalum!Tiketi ni chache!
Hii ni sherehe ya utamaduni, umoja na ubunifu halisi wa Kiafrika. Hapa ndipo sauti za Afrika zinarindima, Sio muziki wa kibiashara, bali midundo halisi, yenye asili ya kiafrika na yenye kusisimua.
Tamasha hili hufanyika katika eneo la kihistoria la Mji Mkongwe,likileta mchanganyiko wa historia na burudani, Muziki unajaza hisia za burudani, taa zinazoleta nuru Mji Mkongwe, na watu kutoka kila pembe ya dunia huunganishwa na midundo ya pamoja. Lakini uzuri wa Busara hauishii jukwaani tu pata fursa kuonja vyakula vya kila namna kutoka pwani ya Zanzibar, mitindo ya mavazi ya Kiafrika, soko la wazi, sherehe za ufukweni, na burudani ya Paredi iliyopangwa kwa umahiri.
Zaidi ya yote, Sauti za Busara ni kwa ajili YAKO.Pata tiketi yako sasa na tutengeneze kumbukumbu isiyosahaulika.
Tiiketi za VIP ni chache, nunua yako mapema na ujipatie Zawadi wakati wa Tamasha.
Tembelea https://busaramusic.org/ kwa maelezo zaidi na kuwa sehemu ya tamasha la kipekee barani Afrika.