Jiandae kwa toleo la 23 la Sauti za Busara litakalowasha moto mitaa ya Stone Town, Zanzibar kuanzia tarehe 5 hadi 8 Februari 2026! Mwaka huu, tunafuraha kutangaza orodha ya wasanii mahiri, wakiongozwa na gwiji wa muziki wa Afrika.
Kwa mara ya kwanza kabisa, Salif Keita, anayejulikana kama “The golden voice of Afrika,” atapanda jukwaani katika tamasha la Sauti za Busara. Onyesho lake litaweka historia si tu kwa tamasha hili bali pia kwa muziki wa Afrika, likiwaunganisha vizazi kupitia sauti, roho, na simulizi. Kutoka moyo wa Mali hadi pwani za Zanzibar, ujio wa Salif Keita unasherehekea nguvu ya urithi wa Kiafrika na roho ya mshikamano inayobeba maana ya Sauti za Busara.
Ataungana na wasanii wengine mahiri na chipukizi kutoka kila pembe ya bara la Afrika na mataifa ya diaspora. Ben Pol (Tanzania), Man Fongo (Tanzania), Pilani Bubu (South Africa), Lindigo (Réunion), Malcolm Jiyane Tree-O (South Africa), Sousou & Maher Cissoko (Senegal & Sweden), Kara Sylla & Baye Fall Band (Switzerland), Hammer Q (Zanzibar), Atanda & Afrojazz Messengers (Nigeria & UK), Tarajazz (Zanzibar), La Carmen Y Su Familia Musical (Colombia), Mehmet Polat Quartet (Netherlands) .
Orodha ya wasanii wengine ni kama Alamokha (Tanzania), Mama C & The Fusion Band (Tanzania), Magomamoto Theatre Group (Tanzania), Man Kifimbo (Tanzania), Labdi (Kenya), Ancestors (Togo), Abdel Grooz (Canada & Algeria), Bilal Irshed Trio (Ghana, Palestine & Denmark), Ahamada Smis (Comoros), Seby Ntege (Uganda), Kaya Byinshii (Rwanda), Rajab Suleiman & Kithara (Zanzibar), DCMA Young Stars (Zanzibar) Swahili Encounters (Various),na wengine wengi!