Loryzine
Tangu mwaka 2008 kikundi cha Loryzine kimekuwa kikipiga muziki wa dansi ukichanganyika na muziki wao wa asili wa visiwa vya Reunion uitwao “Maloya”. Muziki huu unasemekana kuwa umetokea Afrika ya Mashariki na Madagaska wakati wa utumwa.
Loryzine wanapiga muziki wa kuchangamsha watazamaji wao, wao hupenda kuwajumuisha watazamaji washiriki kucheza nao.

