Mamy Kanouté
|
Mamy Kanouté alizaliwa katika familia ya Griot nchini Senegal. Mara kwa mara ameshirikiana na wanamuziki wengi kutoka nchini Senegal kama Youssou N'Dour, Baaba Maal, Omar Pène, na Didier Awadi. Hivi karibuni, Mamy Kanouté aliingiza sauti yake katika sinema ya Black Panther ya nchini Marekani. Hivi sasa anaifanyia kazi albamu yake ya tatu chini ya mtayarishaji kutoka uswizi Fred Hirschy, kazi mpya itakayochukua mahadhi ya hip hop, sauti za kisasa na mivuto ya kieletroniki huku akibaki katika ukweli na kiini cha utamaduni wake. |

