Mehdi Laifaoui Trab Project
|
Mehdi Laifaoui ni msanii mwimbaji, mtunzi kutoka Algeria, muziki wake umechanganyika na Bedouin na trab, muziki wa pentatoniki ambao huipa muziki wa rai wa Algeria ladha ya kipekee ya Afrika. Nyimbo zake nyingi ni nyimbo za asili, na uliosanifiwa kutoka kwenye muziki wa rai wa miaka ya 70 na 80. Muziki wa Mehdi Laifaoui utakusafirisha kwenye safari ya historia ya muziki wa Aljeria ambao unaangazia dunia ya sasa. |

