The Zawose Queens

Country
Festival
Sauti za Busara 2025
Recordings

Maisha, 2024

The Zawose Queens - Maisha (Official Video)
Photo of The Zawose Queens (view larger)
The Zawose Queens

Read in English

Ilianzishwa mwaka 2019 kupitia makazi yaliyofadhiliwa na British Council yaliyoratibiwa na Aziza Ongala, Zawose Queens zinaunganisha wanamuziki wa kike kutoka familia ya Zawose kutoka Tanzania wanaopiga muziki wa jadi na wa kisasa wa kielektroniki wenye kusisimua.

Kundi linaloongozwa na Pendo na Leah, Wasanii wenye talanta wa familia maarufu ya Zawose. Maonyesho yao ya kipekee na yanayovutia yanaonyesha si tu sauti zenye nguvu bali pia vyombo vya jadi kama marimba na ngoma ya kike ya Gogo, muheme. Kabla ya makazi hayo, Pendo na Leah hawakuwa wamewahi kufikiria kuunda kundi, kwani walikuwa wakijikita katika kuhifadhi urithi wa muziki wa familia yao. Hata hivyo, msaada na hamasa walizozipata ziliwapa nguvu ya kuangalia njia ya kutengeneza kundi na kukuza na kuonensha ubunifu wao.

Zawose Queens kwa haraka walivutia watazamaji na sauti yao ya kipekee. Walirekodi albamu yao ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2019, lakini janga la Covid-19 lilichelewesha kutolewa kwake baada ya kusaini na Real World Records mwaka 2021.

Tangu wakati huo, wametumbuiza katika maonyesho 17 katika nchi tano, wakitumbuiza kwenye hatua maarufu kama Glastonbury, WOMAD, na African Oye. Pendo na Leah wanaendelea kuwahamasisha watazamaji, wakihusisha tamaduni na kusherehekea nguvu ya umoja wa muziki. Safari yao ni ushahidi wa mabadiliko yanayotokana na ushirikiano na nguvu endelevu ya urithi wa kitamaduni. Wanapoitazama siku zijazo, Zawose Queens wanaendelea kuutangaza utamaduni wao wa asili kupitia ubunifu wao wa muziki wa kipekee.