Alamokha
Alamokha ni mtunzi, mwandishi wa muziki na mpiga gitaa, ambaye muziki wake ni kielelezo na kitambulisho tosha cha kitamaduni, na kihisia. Akiunganisha mitindo ya Afro Soul, Afro Fusion, na Afro Jazz, anavumbua sauti za kipekee zinazohadithia simulizi za Kiafrika zenye simulizi za uvumilivu, upendo, na matumaini. Wimbo wake wa kutia moyo, “Don’t Give Up”, ni ushahidi wa dhamira yake: kuinua, kuponya, na kuhamasisha kupitia muziki.
Mzaliwa na mkulia Tanzania, Alamokha ni msanii wa kwanza na wa pekee katika ukoo wake wote, ni uthibitisho tosha kwamba ari na mapenzi ya kweli kwa muziki vinaweza kuvuka mipaka ya jadi. Safari yake ya muziki ilianza akiwa na umri wa miaka mitano tu, akijifundisha mwenyewe kwa kutumia msukumo wa ndani na wito wa moyoni. Ingawa familia yake awali haikuelewa shauku yake, Alamokha hakuwahi kuyumba katika ndoto yake.
Baada ya kumaliza sekondari, aliamua kuipa taaluma hiyo uzito zaidi kwa kujiunga na Chuo cha Sanaa TASUBA, ambako kipaji chake kilianza kung’aa. Akiwa katika jamii ya kisanii, aligundua sauti yake ya kipekee na kupenda gitaa, ambalo limekuwa ala yake ya kipekee, na alihitimu mwaka 2019. Ukuaji wake wa kisanii uliendelea katika Action Music Academy, ambako alipata ufadhili wa masomo kupitia taasisi ya Kijerumani, na akaimarika katika uimbaji wa jukwaani, uandishi wa muziki, na masoko ya muziki—akihitimu mwaka 2023.
Umaarufu wake katika tasnia ya muziki Afrika Mashariki umenasibishwa na maonesho ya kuvutia katika matamasha makubwa kama Tamasha la Bagamoyo (2019), October Festival (2022), Ongala Music Festival (2022), Marafiki Festival (2023), na Serengeti Festival (2023).
Akiwa na sauti yenye hisia, na uwezo wa hali ya juu wa kupiga ala moja kwa moja jukwaani, Alamokha huungana kwa undani na hadhira inayotafuta muziki wa kweli, wa kitamaduni, na wenye hisia. Maonesho yake si burudani tu ni safari za kipekee kupitia muziki
Akiwa amevutiwa na wanawake mashujaa wa muziki Afrika kama Angélique Kidjo, Yemi Alade, na Fatoumata Diawara, Alamokha anajichongea njia yake mwenyewe—kwa ujasiri, uhalisia, na bila kujificha kama Mwafrika halisi.
Kwa sasa, yupo mbioni kukamilisha albamu yake ya kwanza.

