Magomamoto Theatre Group
Kikundi cha Magomamoto Theatre Group (MTG) kinatumbuiza majukwaani kwa midundo mbalimbali yenye kusisimua ya ngoma za asili. Mchanganyiko wao wa ngoma za kitamaduni, uimbaji, upigaji na uigizaji huwapa watazamaji maonesho ya kuvutia yanayoleta uhai katika simulizi tajiri za Tanzania, kuanzia hadithi za kale hadi simulizi za kisasa.
MTG ilianzishwa mwaka 2019 na wanafunzi kutoka Chuo cha Sanaa, TASUBA huko Bagamoyo. Kundi hili ni mwangaza hai wa urithi wa kitamaduni wa Kitanzania, huku dhamira yao ikiwa kudumisha, kuelimisha, na kusherehekea sanaa za kitamaduni za Tanzania kupitia fani mbalimbali kama vile muziki, dansi, maigizo, sarakasi, ufundi, na sanaa za maonyesho.
Kupitia maonyesho ya jukwaani yenye mvuto, warsha za kijamii, programu za mashuleni, na ushirikiano wa mashirika ya kimataifa kama Ulaya, Marekani, Nigeria, Afrika Kusini, na India, MTG hueneza roho ya kitamaduni ya Tanzania kote ulimwenguni.
Kuanzia kuvutia hadhira hapa nyumbani hadi kuteka nyoyo za mashabiki wa kimataifa. MTG imeibuka haraka kuwa jina maarufu katika ulimwengu wa Sanaa za Maonesho za kitamaduni. Miongoni mwa maonesho yao ya hadhi ya juu ni pamoja na: The Tanzanian Royal Tour (Marekani, 2022), Dubai Expo (2022), Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania (2021) na mengineyo mengi.
Wamewahi pia kutumbuiza katika matamasha makubwa, makongamano na matukio ya kijamii, wakitumia sanaa yao kuhamasisha mabadilishano ya kitamaduni, mazungumzo, na uelewa baina ya jamii.

