Wito kwa Wasanii: Sauti za Busara 2026

Sauti za Busara ni miongoni mwa matamasha bora barani Afrika, sasa lipo kwenye maandalizi ya msimu wa 23. Kama kawaida tamasha lijalo litafanyika katika viunga vya Mji Mkongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 6 – 8 February 2026.
Maombi ya wasanii yanapokelewa mpaka tarehe 31st Julai 2025
Vipaumbele vitatolewa kwa:
- Muziki wenye utambulisho wa kiafrika.
- Wasanii wa kike, au vikundi vinavyoongozwa na wanawake.
- Vijana, wasanii mpya na vipaji vinavyochipukia
- Muziki wenye ujumbe unaogusa jamii
- Muziki wenye kupigwa mubashara ‘LIVE100%’!
Ili ukamilishe maombi ya ushiriki, tafadhali tuma mahitaji yote yaliyoorodheshwa hapo chini. Maombi yasiyokamilika au yatakayochelewa hayatazingatiwa.
- Wasifu wa kikundi/msanii*
- Link ya wasifu wa Msanii iliyopo kwenye tovuti ya Music in Afrika (www.musicinafrica.net)
- Nyimbo 2 za kusikiliza (Audio) za karibuni tuma kwa njia ya Dropbox au Google Drive
- Video 2 za karibuni za maonyesho ya Mubashara (Live) tuma kwa Dropbox au Google Drive
- Picha mbili zenye kuweza kuchapishwa* (hi-res photo)
- Mfumo wa Jukwaa na Mahitaji ya vifaa (kama itapatikana na kama huna unaweza kutengeneza kupitia https://en.musicotec.com/
Hati zote zinazotumika lazima ziwekewe lebo na kupakiwa kwenye / dropbox / google na ututumie links / viungo pekee, kupitia sehemu za fomu unapotuma maombi yako.
Mwisho wa kupokea maombi ya mahitaji yote ni usiku wa tarehe 31st July 2025
Ikichaguliwa, Sauti za Busara italipa gharama zifuatazo kwa wasanii wanaoshiriki(+ 1 mfanyikazi).
- Malipo ya onyesho
- Pesa ya kujikimu kwa ajili ya chakula na viburudisho
- Malazi mtakapokuwa Zanzibar
- Usafiri kwa ajili ya onyesho lako
- Malipo ya visa, utafidiwa ikiwa utaleta risiti
- Pasi za tamasha zima
- Mualiko wa Movers & Shakers (kongamano linalokutanisha wataalamu wa Sanaa ya muziki), mkutano wa waandishi wa habari na matukio mengine
- Wasifu wa msanii/ kikundi katika kitabu cha tamasha, taarifa za habari, tovuti na mitandao ya kijamii.
- Nembo ya mdhamini wa safari itawekwa kwenye tovui, program ya tamasha na kwenye kurasa za mitanadao ya kijamii.
Jopo la uteuzi litakutana mwezi wa nane mwanzoni kukamilisha orodha ya wasanii kwa ajili ya Sauti za Busara 2026. Wasanii wote watajulishwa matokeo kabla ya mwezi wa tisa. Wasanii kutoka nje ya Afrika Mashariki wanatakiwa kutafuta wadhamini wa kuwasafirisha kuja na kuondoka Zanzibar na tamasha litasaidia pale inapowezekana.