Wito kwa Wasanii: Sauti za Busara 2027

Sauti za Busara ni miongoni mwa matamasha bora barani Afrika, sasa lipo kwenye maandalizi ya msimu wa 24. Kama kawaida tamasha lijalo litafanyika katika viunga vya Mji Mkongwe, Zanzibar kuanzia tarehe 11 – 14 March 2027.
Maombi ya wasanii yanapokelewa mpaka tarehe 30th Juni 2026
Vipaumbele vitatolewa kwa:
- Muziki wenye utambulisho wa kiafrika.
- Wasanii wa kike, au vikundi vinavyoongozwa na wanawake.
- Vijana, wasanii mpya na vipaji vinavyochipukia
- Muziki wenye ujumbe unaogusa jamii
- Muziki wenye kupigwa mubashara ‘LIVE100%’!
Ili ukamilishe maombi ya ushiriki, tafadhali tuma mahitaji yote yaliyoorodheshwa hapo chini. Maombi yasiyokamilika au yatakayochelewa hayatazingatiwa.
- Wasifu wa kikundi/msanii*
- Link ya wasifu wa Msanii iliyopo kwenye tovuti ya Music in Afrika (www.musicinafrica.net)
- Nyimbo (Audio) zilizorekodiwa kwa mfumo wa MP3 zenye ubora wa 320kbps
- Linki mbili za Video za hivi karibuni za maonyesho mubashara (Live)
- Picha mbili zenye kuweza kuchapishwa* (hi-res photo)
- Mfumo wa Jukwaa na Mahitaji ya vifaa (kama itapatikana na kama huna unaweza kutengeneza kupitia https://en.musicotec.com/
Nyaraka zote ziwekwe majina kiufasaha na zipakiwe (uploaded) kwenye sehemu husika katika ya fomu ya maomb
Mwisho wa kupokea maombi ya mahitaji yote ni usiku wa tarehe 30th Juni 2026
Sauti za Busara italipa gharama zifuatazo kwa wasanii watakaoshiriki (+ 1 mfanyikazi/ meneja).
- Malipo ya onyesho
- Pesa ya kujikimu kwa ajili ya chakula na viburudisho
- Malazi mtakapokuwa Zanzibar
- Usafiri kwa ajili ya onyesho lako
- Malipo ya visa, utafidiwa ikiwa utaleta risiti
- Pasi za tamasha zima
- Mualiko wa Movers & Shakers (kongamano linalokutanisha wataalamu wa Sanaa ya muziki), mkutano wa waandishi wa habari na matukio mengine
- Wasifu wa msanii/ kikundi katika kitabu cha tamasha, taarifa za habari, tovuti na mitandao ya kijamii.
- Nembo (logo) ya mdhamini wa safari itawekwa kwenye tovui, program ya tamasha na kwenye kurasa za mitanadao ya kijamii.
Jopo la uteuzi litakutana mwezi wa saba mwanzoni kukamilisha orodha ya wasanii kwa ajili ya Sauti za Busara 2027. Wasanii wote watajulishwa matokeo kabla ya mwezi wa tisa. Wasanii kutoka nje ya Afrika Mashariki wanatakiwa kutafuta wadhamini wa kuwasafirisha kuja na kuondoka Zanzibar na tamasha litasaidia pale inapowezekana.
