Salamu za Mwisho wa Mwaka

Disemba 2023

Habari Familia ya Busara, 

Siku zinasogea kwa kasi na tamasha letu pendwa ambalo tumekuwa tukiliandaa kwa mwaka mzima linakaribia. Matarajio ni makubwa kwani orodha ya wasanii itasindikiza siku tatu za muziki wa kiafrika chini ya anga ya Afrika. 

Ili kufanya tamasha kuwa endelevu, tumeanzisha mpango mpya ambapo hoteli zinatoa vyumba vitakavyouzwa  kupitia tovuti yetu, na mapato yote yanakwenda moja kwa moja kusaidia tamasha! Tuna idadi ya vyumba vichache kwa sasa, vinavyoweza kununuliwa kupitia mfumo wetu wa mauzo ya tiketi. Mauzo ya vyumba yameshaanza na yatakayokupa wakati ambao hutousahau katika msimu wa tamasha.

Fanya booking ya chumba hapa !

Tunashirikiana na Kenya Airways kukupatia punguzo la bei za tiketi zote za ndege kwa asimia ishirini kwa abiria wanaokuja kwenye tamasha la Sauti za Busara ili iwe nafuu kwako kuhudhuria tamasha kwa kutumia msimbo wa hati punguzo (promo code SAUTI24)  

Tangu tulipotangaza orodha yetu ya wasanii Tiketi za VIP na nyinginezo zinauzwa haraka, hivyo hakikisha unajipatia tiketi yako mapema tiketi yako! 

Matamasha makubwa ya muziki kama letu yanachangia kwa kiasi kikubwa ongezeko wa hewa  ukaa kutokana na ongezeko kubwa la watu wanaotoka sehemu mbalimbali. Ili kukabiliana na changamoto hii na kupunguza mchango wa kaboni Sauti za Busara, kwa kushirikiana  taasisi ya STAWI kupitia programu ya Roots & Shoots ya Jane Goodall zitasaidia kurejesha msitu wa asili Zanzibar. Jiunge nasi na tusaidie kupunguza athari kwenye mazingira yetu! Unaponunua tiketi yako ya tamasha na malazi, tafadhali nunua pia mti mmoja au wawili (kwa kupitia ukurasa wa tiketi wa Pesa-Pal) ambayo itapandwa Zanzibar baada ya tamasha kusaidia kupunguza hewa ya kaboni. 

Toa mchango wa miti hapa !

Tunakukaribisha kwa furaha wewe, marafiki zako, na wapendwa wako kwenye tamasha lijalo la kusisimua la Sauti za Busara.  Chini ya uongozi mpya, tutafurahi sana kuungana tena pamoja ndani ya Zanzibar kwenye siku tatu za burudani ya aina yake. 

Uongozi wa Busara unawatakia heri na kuwakaribisah nyote kwenye Tamasha mwezi wa Februari. 

Wako,

Timu Busara

Tiketi za mapema zinapatikana hadi tarehe 31 Januari. Nunua Pasi ya Tamasha pamoja na siku tatu za hoteli katika msimu wa Tamasha, na pia panda mti kutusaidia kupunguza athari ya hewa ya kaboni Zanzibar! 

Kata tikiti yako ya tamasha, pata hoteli, na toa mchango wako wa mti hapa!
Sauti za Busara Partners & Supporters
image
Ignite Culture
CRDB Bank Logo
Kenya Airways Logo
Emerson Zanzibar
Stawi Selection Logo
Volks House
Zanlink Logo (without LT) CMYK copy-1.png
Sauti za Busara - One Africa

Follow us on Social Media to get the latest updates:

This e-mail has been sent to [[EMAIL_TO]], click here to unsubscribe.

Busara Promotions. Maisara, Stone Town 3635 Zanzibar City TZ