Results: 1 to 1 of 1
Hanitra
Country Madagascar Genres acoustic Website www.hanitra.com Festival Sauti za Busara 2012 Recordings 📼 Any Aminay (2010)
Hanitra ni mwimbaji na mpiga gitaa kutoka kisiwa cha Madagascar. Misingi ya nyimbo zake unatokana na haiba ya muziki ya Madagascar, pamoja na vionjo kutoka Cuba na Brazil, alichukua nyimbo za asili kwa nguvu na hatimaye kuwakilisha kizazi cha Malagasi. Sauti ya kuvutia ndio iliyomfanya kuwa mmoja kati ya wasanii ambao uchukuliwa kama mwimbo wa taifa wa Madagascar.
Hanitra alianza kuimba na kupiga gitaa alipokuwa na umri wa miaka saba. Mwaka 1979, alishiriki katika shindano la kitaifa ambapo kipaji chake kiligunduliwa rasmi na kujiunga na bendi moja kwa moja ya Lolo Sy Ny Tariny. Alienda Ufaransa akitokea Madagascar. Mwaka 1997 alirudi Madagascar. Kwa sasa anaishi katika kisiwa cha Reunion na ana shauku kubwa ya kuburudika na mashabiki wake wote katika ukanda wa Bahari ya Hindi.