Results: 1 to 1 of 1
Nawal & Les Femmes de la Lune
Country Comoros Mayotte Genres acoustic fusion roots spiritual Website www.nawali.com Festival Sauti za Busara 2009, 2013 Recordings 📼 Kweli, 2001; Aman, 2007; Nawal & Les Femmes de La Lune, 2010 (CD/DVD); Embrace the Spirit, 2011
Nawal ni mzaliwa wa Komora aliyetokea katika familia ya wanamuziki, Nawal alianzakuonyesha kipaji cha muziki alipokuwa ana umri mdogo. Amehamia nchini Ufaransa na kufanikiwa kuwa kama nembo ya utambulisho wa visiwa vya Komoro.
Nawal anaweza kupiga vifaa aina tofauti vya muziki kama Gitaa, Gambusi (kinanda cha asili ya Yemen) ngoma, na vifaa vingine vya muziki. Namal aliwahi kusema katika mahojiano kwamba “ Kifaa changu cha mwanzo kabla ya vyote ni Sauti”
Nawal ana uwezo wa kushika nyoyo za watu kutokana na sauti na ujumbe anaoutoa kupitia sanaa yake ya muziki. Nawal huchanganya muziki wa asili na kutia vionjo vya kisasa ili kuhakikisha kila mtu anaridhika na kazi yake, na tunategemea kumuona tena akiwa na akina dada kutoka Komora katika tamasha la Sauti za Busara 2013.
With thanks to Conseil General de Mayotte