Sahra Halgan Trio
Country Somaliland Genres traditional pop fusion Website athosbook.com Festival Sauti za Busara 2017 Recordings 📼 Somaliland, 2009; Faransiskiyo Somaliland, 2015
Sahra Halgan ni muimbaji mwenye sauti nyororo kabisa. Nyimbo zake zina mahadhi ya kisomali ambayo yanakaribiana sana na mahadhi ya kisudani na nchi nyengine za uarabuni.
Takriban Sahra Halgan huwa anaimba na kupiga makofi tu bila ya kinanda cha aina yoyote. Lakini hivi karibuni amekuwa akishirikiana na wanamuziki wawili wanaotoka Ufaransa, ambao ni Aymeric Krol na Mael Saletes na wanapiga muziki wanaouita ‘Muziki mchanganyiko kutoka Somaliland’
Sahra aliondoka Somalia wakati wa vita vya mwaka 1993 na kukimbilia Ufaransa. Wakati huo nchi iligawanyika kati ya wale waliokuwa wakampinga Siad Barre na wale waliokuwa wanamuunga mkono. Watu wa kaskazini ya nchi wakajibagua na kujiita Somailand. Na huko ndipo kwao Sahra Halgan.
“Nilianza kuimba nikiwa nina miaka kumi na tatu, wakati huo Somalia ilikuwa ni nchi ya amani kabisa” alisema Sahra. “Na wakati vita vilipoanza nilijitolea kama ni mhudumu msaidizi wa madaktari, japo kuwa sikuwa nina elimu ya udaktari, nikitumia sanaa yangu kuwaliwaza waliojeruhiwa.” Aliendelea kusema
Wakati wa utawala wa Siad Barre, watu walikatazwa kuimba na kupiga ngoma. Halgan akaanza kuimba nyimbo za kimapinduzi. Halgan alianza kuimba nyimbo za kumpinga dikteta Barre, na akienda kutembelea kambi zilizopo misituni, ambapo majeruhi walikuwa wanatibiwa. Akenda huko kuimba nyimbo za kimapinduzi na kuwahamasisha wapiganaji.
Baada ya kuishi Ufaransa kwa miaka mingi, Sahra Halgan alirudi Hargeisa, mji mkuu wa Somaliland na kufungua studio ambazo ndio za pekee mjini humo, na wasanii wote wanatumia studio hizo. “Madhumuni ya studio hizi ni kulitangaza jina la Somaliland lijulikane kote, tukumbukwe na watu wote duniani kama Somaliland ni nchi tofauti na Somalia. Na ni nchi ya amani, ina wananchi million nne”. Alisema Sahra Halgan
with thanks to Baam Productions and CNV
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava