Kidumbaki JKU
Country Zanzibar Genres coastal roots Festival Sauti za Busara 2012 Kidumbaki ni maarufu sana katika kisiwa cha Unguja na moja kati ya ngoma zenye asili ya Zanzibar. Kikundi cha JKU kilianzishwa rasmi mwaka 2000 na kufanikiwa kuongeza sifa zake kila mwaka na sasa kuwa kikundi maarufu sana katika vitongoji vyote vya Zanzibar kwa kila umri kutokana na aina yao ya uchezaji ambayo hunogeshwa kwa kutumia kiuno.
Kidumbaki hupendwa na watu wengi, katika sherehe za harusi, sherehe za siku za kuzaliwa na sherehe nyingine tofauti muimbaji huimba kutokana na tukio husika. Kidumbaki kinaweza kupigwa kuanzia saa moja mpaka saa nne au tano kwa kuunganisha nyimbo na kivutio kikubwa pale muimbaji anapoimba na watazamaji kuitikia.
Kidumbaki cha kisasa hutumia nyimbo za taarabu zenye kupendwa. Tofauti na taarab, kidumbaki hutumia sana mtiririko wa utunzi kuliko ushairi wa nyimbo za taarab, mara nyingi huwakosoa watu kuhusu upotofu wa maadili. Katika ujumbe , wanatunga mashairi kutokana na sherehe husika na kutuma ujumbe maridhawa kwa jamii.
Algeria Angola Australia Austria Benin Burkina Faso Burundi Cameroon Canada Cape Verde Comoros Congo Côte d'Ivoire Denmark DRC Egypt eSwatini Ethiopia Far East Finland France Gambia Germany Ghana Guinea Guinea Bissau Iraq Japan Kenya Lesotho Madagascar Malawi Mali Mauritania Mauritius Mayotte Morocco Mozambique Namibia Netherlands Nigeria Norway Pan Africa Pemba Puerto Rico Reunion Rwanda Senegal Seychelles Somaliland South Africa Sudan Suriname Sweden Switzerland Tanzania Uganda UK USA Various Yemen Zambia Zanzibar Zimbabwe
acoustic acrobats afrobeat band blues bongo flava coastal comedy dance dj electro fusion hiphop jazz kidumbak pop reggae rock roots rumba spiritual spoken word taarab traditional urban zenji flava