HATUA MOJA MBELE, MBILI NYUMA

Busara Promotions ni taasisi isiyo ya kiserikali linalotangaza tamaduni tofauti na kutoa fursa za ajira za kitaaluma katika tasnia ya muziki ndani ya Afrika Mashariki kwa kubadilishana na kanda nyingine. Tukio lake kuu ni Sauti za Busara, tamasha la muziki la kiAfrika ambalo limekuwa likifanyika Zanzibar mwezi wa Februari kila mwaka tangu 2004 (isipokuwa 2016).

Gharama za uendeshaji wa taasisi kwa mwezi ikiwa ni pamoja na mishahara na kodi ya ofisi, ni dola za kimarekani elfu 10k, ambazo zililipwa na Ubalozi wa Norway kuanzia 2009 hadi Machi 2022. Tangu Aprili 2022, taasisi ilisaini makubaliano ya miaka 3 ya ufadhili na Pennyroyal Ltd., linalofanya biashara kama Blue Amber Zanzibar. , makubaliano yaliyotarajiwa kumalizika Machi 2025.

Mkataba wa ukodishaji wa ardhi wa miaka 99 kwa Blue Amber umesitishwa na mamlaka za serikali, ikiwa ni pamoja na amri ya kusitisha ujenzi kutokana na mzozo wa ardhi unaoendelea. Mnamo tarehe 30 Agosti, Busara Promotions ilipokea taarifa rasmi ya kusitishwa mara moja kwa udhamini wa Blue Amber.

Kwa mara nyingine tena, hatuna uhakika kwa taasisi kuendelea kuwepo kwani hakutokuwa na pesa za uwendeshaji wa taasisi baada ya mwezi wa Septemba.

Maandalizi ya tamasha la 20 la Sauti za Busara litakalofanyika 2023 yalikuwa yanaendelea vizuri. Wanamuziki kutoka Bara zima walithibitisha kushiriki, tiketi zilianza kuuzwa na shauku ya tamasha ikiongezeka.

Kama wote tunavyofahamu, Sauti za Busara huleta manufaa makubwa kijamii, kiutamaduni na kiuchumi ndani ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Wafadhili na wahisani wa tamasha wanahakikishiwa fursa ya kujitangazwa kupitia majukwaa mbalimbali ya habari; tafadhali wasiliana nasi kwa haraka ikiwa una nia ya kushirikiana nasi.

Majadiliano ya dharura yanaendelea, na mamlaka za serikali, viongozi wa biashara na taasisi za umma. Tarehe 15 Septemba, Bodi na Uongozi wa Busara Promotions watafanya uamuzi ya mwisho kama inawezekana kuendelea au la.

Iwapo tamasha italazimika kuhairishwa, wale wote ambao tayari wamenunua tiketi watarudishiwa malipo yao kikamilifu.

Yusuf Mahmoud

CEO & Festival Director