UJUMBE KWA MARAFIKI, WADAU WOTE WA SAUTI ZA BUSARA NA KWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Shukran za dhati kwa kutufariji na kututia moyo. Tumesikia na hatutakata tamaa! Waandaji wa tamasha wamejitolea kuhakikisha tamasha linaendelea.

Hivyo, tunatoa wito kwa mashirika ya umma, sekta binafsi , mashirika ya ndani na ya kimataifa, balozi na watu binafsi kudhamini tamasha la Sauti za Busara. Tuungane Kwa Pamoja kuendelea kuleta maelfu ya wageni Zanzibar, kutengeneza ajira na urafiki, kukuza na kuutangaza muziki wa ndani na Afrika Mashariki duniani kote. Tunahitaji msaada wako kuendelea kuandaa moja kati ya matamasha bora zaidi ya Muziki Barani Afrika, na kuleta watu pamoja kusherehekea tunayojivunia zaidi Zanzibar na Tanzania: ukarimu, muziki na urafiki, ambavyo vina nguvu zaidi kuliko shida na tofauti zetu.

Tunahitaji kukusanya pesa za kutosha katika wiki zijazo. Tunaamini utaunga mkono jitihada zetu kadri uwezavyo. Fursa ya kutangaza biashara inatolewa kwa washirika wote.

Tafadhali ungana nasi kufanikisha tamasha la 20 liwe bora zaidi!

Tofauti Zetu, Utajiri Wetu!

Je, ungependa kufadhili? Bonyeza hapa