Serikali ya Mapinduzi kushirikiana na wadau kuendeleza Sauti za Busara

by Azam Tv, Oct 17, 2022 

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Zanzibar, Simai Mohamed Said amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuendeleza tamasha la Sauti za Busara ili kusaidia ukuaji wa sekta ya utalii na kukuza uchumi wa Zanzibar. Waziri Simai ameyasema hayo baada ya kushuhudia utiaji saini ya udhamini wa miaka miwili na nusu wa Tamasha la busara kati ya kamapuni CPS Fumba town na Busara Promotions.